Na: Mwandishi wetu

Mwenyekiti wa Bunge wa masuala ya Ukimwi, Rwegasira Oscar,  amesema wabunge wanatarajia kupima Ukimwi kwa hiyari Alhamisi Juni 21 shughuli itakayoenda sambamba na mjadala wa wazi juu ya ugonjwa huo. 

 

Akizungumza na waandishi wa habari  jana Juni 19, 2018, jijini Dodoma, Oscar amesema mjadala huo utahudhuriwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na wabunge.

Bofya hapa kwa Habari zaidi.....

 

          
 Picha na mtandao       

Na: Tatyana Celestine

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, SUA, kupitia kituo cha Utafiti wa Ufuatiliaji wa Magonjwa Ambukizi cha kusini mwa Afrika, SACIDS, kimepokea ombi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo DRC, kutuma timu ya wataalamu kwenda kusaidia kukabili ugonjwa wa Ebola uliozuka nchini humo hivi karibuni.

Hayo yameelezwa na Mtafiti kiongozi kutoka SUA, Prof Ezron Karimuribo alipokuwa akijibu swali kuhusu nafasi ya  mpango-maombi wa Data-Afya kukabiliana na hatari ya ugonjwa wa Ebola uliozuka huko DRC, usiingie nchini na kuhatarisha afya za watanzania.

Bofya hapa kwa Habari zaidi.....

Subcategories

TOA MAONI YAKO HAPA