Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael T. Chibunda  wa pili kushoto pamoja na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Elimu na Taaluma wa pili kulia, na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Tawala na Fedha wa kwanza kulia wakifuatilia maelezo kuhusu kitengo cha Sayansi ya Udongo wakati wa maandalizi ya maonesho ya Vyuo Vikuu chuoni hapo.(Picha na Tatyana Celestine Manda).   

Na Tatyana Celestine                

Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kina kila sababu ya kushinda katika maonesho ya Vyuo vikuu kutokana na umahiri wake katika Teknolojia,Utafiti na kozi bora zinazolibeba Taifa kwa upekee wake katika kujenga Tanzania ya viwanda.

Hayo yamesemwa na  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael T. Chibunda  wakati wa maandalizi ya kushiriki maonesho hayo chuoni hapo, siku mbili kabla ya maonesho hayo kuanza na kusema kuwa watanzania wajitokeze kwa wingi  kushiriki kwa lengo la kufaidika na uwepo wa SUA katika maonesho hayo ambayo yatafanyika jijini Dar es salaam.

Bofya hapa kwa Habari zaidi.....

 

Mradi wa mbinu shirikishi katika uzalishaji wa nyanya (IPM) unaodhaminiwa na USAID unaohusu kutotumia madawa katika kilimo cha mbogamboga. (Picha na Tatyana Celestine)   

 

Na, Tatyana Celestine

Wakulima nchini wametakiwa kuacha kutumia viatilifu katika kilimo cha mboga mboga ili kujiepusha na madhara yatokanayo na viatilifu hivyo kwani ni sumu katika mwili wa binadamu na kuleta athari katika mazingira.

 

Hayo yamesemwa na Afisa kilimo mazao ya bustani toka Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kitengo cha HORTCULTURE BW.GODWIN RWEZAULA katika maandalizi ya kutoa mafunzo kwa wakulima wengine ambayo itaambatana na kukamilisha mradi wa mbinu shirikishi katika uzalishaji wa nyanya (IPM) unaodhaminiwa na USAID unaohusu kutotumia madawa katika kilimo cha mbogamboga.

Bofya hapa kwa Habari zaidi.....

       

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Taaluma Prof.Peter Gillah akitoa neno kwenye semina iliyoandaliwa na chuo hicho kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Kilimo nchini China kwa maafisa ugani na kilimo kutoka mkoa wa Morogoro na Dodoma.PICHA NA ALFRED LUKONGE

 

                     

Na:Alfred Lukonge 

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA upande  wa Taalauma Prof. Peter Gillah amesema kuwa chuo hicho kimepewa jukumu na Mh. Rais Dkt. John Magufuli la kuongoza utekelezaji wa Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP 2) kupitia wataalamu wake mbalimbali waliomo chuoni humo.

Prof.Gillah amebainisha hayo kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo wakati wa uzinduzi wa semina iliyoandaliwa na SUA  kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Kilimo cha nchini China kwa maafisa ugani na kilimo kutoka mkoa wa Morogoro na Dodoma.

Bofya hapa kwa Habari zaidi.....

 

 

Subcategories

TOA MAONI YAKO HAPA