Na:Ayubu Mwigune

Timu ya taifa ya Tanzania inatarajia kuondoka leo kuelekea nchini Rwanda kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Rwanda, mchezo ambao unasubiriwa kwa hamu na mashabiki wengi wa soka nchini ili kuona hatima ya timu hiyo ya Taifa star.

Kikosi hicho cha timu ya taifa ya Tanzania kitasafiri kwa usafiri wa ndege  ya AIR TANZANIA na kupitia jijini dar es salaam, kikitokea jijini mwanza ambako kiliweka kambi .

Image result for taifa stars logo

Picha na mtandao.

Katika mchezo wa awali ambao ulikutanisha timu hizo ulishuhudia timu hizo zikitoka sare ya goli 1-1 ,taifa stars inahitaji matokeo ya ushindi wa aina yeyote ama  sare 2-2 ili kuhakikisha wanatengeza nafasi ya kusonga mbele.

 

TOA MAONI YAKO HAPA