Na Rajabu Kimaro

Kocha msaidizi wa clabu ya Simba ya Dar es salaam Jackson Mayanja amesema kuwa klabu yake bado inakabiliwa na tatizo la umaliziaji katika safu ya ushambuliaji.

Kauli hiyo ya mayanja imekuja baada ya timu yake kulazimishwa sare ya kutofungana dhidi ya timu ya Mlandege ya zanzibar katika mchezo wa kirafiki ikiwa ni mwendelezo wa michezo yake ya kujiandaa na ligi kuu Bara pamoja na mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya mahasimu wao wakubwa timu ya Yanga unaotarajiwa kuchezwa tarehe 23 mwezi huu.

Tokeo la picha la simba  vs ryon


                                                                                                                           Picha na mtandao.

 

Licha ya kauli yake hiyo lakini kocha huyo amewatoa hofu mashabiki wa klabu hiyo kwa kusema mchezo wa mpira hautabiriki kwa hiyo ana imani na timu yake  na anaamini watashinda katika mchezo huo wa ufunguzi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.

TOA MAONI YAKO HAPA