MICHUANO YA NETBALL LIGI DARAJA LA KWANZA KITAIFA MKOANI MOROGORO.

Na: Suzane Cheddy

Katika michuano ya kitaifa ya netiboli inayoendelea mjini Morogoro, timu ya Polisi Arusha imeibuka na ushindi wa magoli 59 kwa 56 dhidi ya timu ya Tumbaku Morogoro.


Akizungumza na SUA MEDIA mwenyekiti kamati ya ufundi taifa Asha Sapi amesema kuwa michuano imeanza vizuri kutokana na wachezaji wote kuonyesha ushindani katika uchezaji pamoja na nidhamu kwa waamuzi.

Sapi amesema licha ya changamoto zinazozikabili timu mbalimbali na kupelekea ushiriki mdogo wa timu za netball ambapo timu 11 ndizo zimefanikiwa kushiriki michuano huku timu 10 zikishindwa kutokana na ukosefu wa fedha.

Hivyo ameomba serikali na taasisi mbalimbali kujitokeza kudhamini mchezo huo wa netiboli ikiwa ni moja ya kukuza vipajiĀ  pamoja na kuimarisha afya.

Save

Save

TOA MAONI YAKO HAPA