Na: Fadhila Kizigo   

Timu ya Netball  Uhamiaji imeibuka na ushindi katika michuano ya ligi daraja la kwanza iliyofanyika mkoani Morogoro huku   Naibu Waziri wa Habari ,Sanaa,Utamaduni na Michezo  Mh. Anastazia Wambura  akitoa wito kwa wanawake kushiriki michezo ya Netball.

Uhamiaji imeibuka kidedea kwa kufunga magoli 776 kati ya michezo kumi waliyocheza na kufanikiwa kuwa mshindi wa michuano hiyo wakifuatiwa na timu ya Polisi Morogoro.

Wachezaji wa timu ya Uhamiaji wakiwa na kombe lao walipoenda kuliwasilisha katika makao makuu ya idara hiyo Kurasini jijini Dar es Salaam.( Picha na mtandao)

Akizungumza na waandishi wa habari kiongozi wa timu ya Uhamiaji Jaqline Sikozi amesema kuwa ushindi wao nikutokana na ushirikiano wao uwanjani na mazoezi ya mara kwa mara.

Jaqline amesema kuwa ushindi walioupata unajenga uzoefu wa  mashindano ya Muungano yanayofuata na kutegemea ushindi tena kwa Uhamiaji.

Kwa upande wa Naibu Waziri Wambura amewapongeza wote walioshiriki michuano hiyo licha ya kukumbwa na ukata wa fedha .

Save

TOA MAONI YAKO HAPA