WACHEZA SOKA GHALI DUNIANI

Na:Adam  Ramadhan
Mchezo   wa  Soka  kwa  sasa  ndio   umekuwa  mchezo  wenye  gharama  zaidi  duniani  hasa  katika  manunuzi  ya  wachezaji, lakini  pia  ndio  mchezo  wenye  mashabiki  wengi  zaidi  ulimwenguni  kwa  sababu  umekuwa  na  mvuto  sana.


SUAMEDIA  inakuletea  orodha  ya  wachezaji   walionunuliwa  kwa  bei  ghali  zaidi  duniani  mpaka  sasa, Paulo  Pogba  amesajiliwa  kutoka  Juventus  kwenda  Manchester  United  kwa  ada paundi  milioni 89 na  kuwa  mchezaji  ghali zaidi  duniani  kwa sasa.

                              Paul Pogba mchezaji anayeshikilia rekodi ya kununuliwa bei ghali duniani kwa wachezaji wa mpira wa miguu. ( Picha na mtandao)

 Gareth Bale  alisajiliwa   kutoka  Tottenham Hotspurs   kwenda  Real  Madrid  kwa ada ya  paundi milioni 85, Mreno  Cristiano  Ronaldo  alisajiliwa  kwa  ada  ya  paundi  milioni  80  kutoka  Manchester  United  kwenda  Real  Madrid   mwaka  2009.


Mwaka  2001  AC milan  walimuuza  Ricardo  Kaka  kwenda  Real  Madrid  kwa  ada  ya  paundi  milioni  56, Lakini  Real  Madrid  wakamsajili  Zinedine  Zidane mwaka  2001  kutoka  Juventus, Barcelona  wakamuuza  Luis  Figo  kwenda  Real  Madrid kwa ada ya paundi milioni 37.


Hernan  Crespo  alisajiliwa  kwa  paundi  milioni  35.5  kutoka  Parma  kwenda  Lazio  mwaka  2000, Denilson   akasajiliwa  kutoka  Sao  Paolo  kwenda  Real  Madrid  kwa  ada  ya  paundi  milioni  32,  mwaka 1997 Barcelona  wakamuuza  Ronaldo  kwenda  Intermilan kwa  ada  ya  paundi  milioni  19.5.


Mnamo  mwaka  1996  Blackburn  walimuuza  Alan  Shearer  kwenda  Newcastle   kwa  ada   ya   paundi  milioni 15, Maradona  akauzwa  kutoka  Boca Junior  kwenda  Intermilan kwa  ada  ya  paundi  milioni 3.0  mwaka  1982.


Paulo  Rossi  mwaka  1976   akauzwa  kwa  ada  ya  paundi  milioni  1.75   kutoka Vicenza kwenda  Juventus, Napoli  wakamchukua  Giuseppe  Savoldi  kutoka  Bologna  kwa  ada ya paundi  milioni 1.2, Paundi 922,000 ikatumika  kumsajili Johan  Cruyff  kutoka  Ajax  kwenda  Barcelona.
Mnamo  mwaka  1873  Willie  Groves  alisajiliwa  na  Aston  villa  akitokea Westbromwich  Albion  kwa  ada  la  paundi  100.

TOA MAONI YAKO HAPA