KILIMANJARO QUEEN FAINALI LEO CHALENJI

Na:Adam   Ramadhan

Timu ya Soka ya Wanawake Tanzania Bara, Kilimanjaro Queens, leo inatarajiwa kuvaana na Kenya katika mchezo wa fainali wa Kombe la Chalenji kwenye Uwanja wa Ufundi uliopo Njeru, mjini Jinja huko nchini Uganda.

Timu hiyo ya Bara ilitinga fainali baada ya kuwatoa wenyeji Uganda katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa mwishoni mwa wiki, ikishinda 4-1 huku nayo Kenya kwa upande wake ikiitoa Ethiopia katika mchezo mwingine wa nusu   fainali.

                                      Timu ya Soka ya Wanawake Tanzania Bara Kilimanjaro Queens(Picha na mtandao)

 

Kuelekea mchezo wa leo, Kilimanjaro Stars inapewa nafasi kubwa ya kuibuka mabingwa wa michuano hiyo kutokana na kandanda walilolionyesha hatua zilizopita ikiwa na wakali wake kibao kama vile Donosia Daniel, Mwanahamisi Omari, Stumai Abdallah na Asha Rashidi ambao ndio walipachika mabao kwenye mchezo wa nusu fainali dhidi ya Uganda.

Kabla ya mchezo huo wa fainali, kutakuwa na mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu kati ya Ethiopia na Uganda.

TOA MAONI YAKO HAPA