SAMMATA HATARI ZAIDI DAKIKA YA 20 ZA MWISHO

Na:Adam  Ramadhan

Mshambuliaji Mbwana Samatta kutoka Tanzania  anayeichezea  klabu  ya  KRC Genk  ya Ubelgiji  tayari  amefikisha  mabao sita ukijumlisha yale ya Ligi Kuu ya Ubelgiji pamoja na michezo ya ligi ya  Europa.

Sammata  amefunga mabao hayo sita, mawili ni ya Europa na manne ni ya ligi lakini inaonekana  Samatta ni hatari zaidi katika dakika za mwisho hasa  akiingia  wakati  wa  mabadiliko.

 

                                                         Mbwana Samatta mwenye jezi Nyekundu katikati. Picha na mtandao

Katika mabao hayo sita, ni bao moja tu dhidi ya Oostende katika mechi iliyochezwa Julai 31, ndilo alilofunga  katika dakika ya 10 ya mchezo na mabao mengine yote, amefunga kuanzia dakika ya 73 hadi 80, hali inayoonyesha kuwa kila dakika 20 za mwisho, ni mtu wa kuchungwa kwelikweli.

 

Mabao aliyofunga katika mechi za Europa ni dhidi ya NK Lokomotiva, alifunga katika dakika ya 83 na mechi ikaisha kwa sare ya mabao 2-2. Mechi ya pili dhidi ya timu hiyo, akafunga pia katika dakika ya 80.

TOA MAONI YAKO HAPA