Na:Ayoub Mwigune

Benchi la ufundi la klabu ya Azam fc limeelezea hali  ya maendeleo ya  wachezaji wake wawili ambao walikuwa majeruhi kutokana na kuchanika misuli ya nyama za paja kuwa tayari wote wawili tayari wameshaanza mazoezi mepesi hali inayoonesha kwamba wanaendelea vyema .

 

Akizungumza na tovuti ya klabu hiyo Daktari wa timu hiyo MWANANDI MWANKEMWA amesema licha ya kuanza mazoezi hayo lakini nahodha wa timu hiyo JOHN  BOCO yeye atakuwa chini ya uangalizi na huenda wiki mbili zijazo akawa yupo fiti na kurejea uwanjani.

 

                                                                                                          PICHA NA MTANDAO.   

 

AZAM FC wanatarajia kucheza na klabu ya MTIBWA SUGAR siku ya ijumaa tarehe 24/2/2017 katika michuano ya kombe la F.A mchezo ambao utachezwa katika uwanja wa CHAMANZI majira ya saa moja usiku kwa saa za afrika mashariki.

TOA MAONI YAKO HAPA