Na:Adam Ramadhani

Klabu  ya  Manchester  United  imefanikiwa  kutwaa  kombe la  ligi  la ndani yaani  EFL baada  ya  hapo  jana kuweza  kuinyuka  klabu  ya  Southamtoni huku  Zlatan  Ibrahimovic  akiwa  shujaa  wa mtanange  huo.

Mchezo  huo  uliofanyika  katika  uwanja  wa Wembley  na  kushuhudiwa   na mashabiki zaidi ya  85 elfu timu  hiyo  ikiwacharaza  Southamptoni  Jumla ya  magoli 3-2 ,magoli  yakifungwa  na Zlatan Ibrahimovic  dakika  ya  19  na 87 huku Jese  Lingard  akifunga  dakika  ya 38.

 

                                                                                                                               Picha na mtandao.

Kwa upande  wa  Southampton  magoli  yaliwekwa  kimiani  na  Manolo Gabbiadini  dakika  ya  45 na  48.

Hoze  Mourinho THE SPECIAL ONE amekuwa  kocha wa  Kwanza kuchukua  kombe  hilo  baada  ya  makocha  watatu  waliotangulia  kushindwa  kufanya  hivyo, Manchester United  imeonekana  kuwa  katika  kiwango  bora  baada ya  kufanya  vizuri  katika   makombe  ya  UEFA ndogo na  Kombe  la  FA.

TOA MAONI YAKO HAPA