AZAM YAELEKEZA NGUVU ZAIDI KWENYE MICHUANO YA LIGI KUU NA KOMBE LA FA

Na:Ayoub Mwigune

Kocha Mkuu wa  klabu ya Azam FC, Aristica Cioaba,  ameweka wazi kuwa wameshasahau yaliyopita na nguvu zao kwa sasa wanazielekeza katika michuano ya Ligi Kuu na Kombe la FA, ili kuhakikisha wanapata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa mwakani.

Kocha huyo wa azam fc amesema kupitia  tovuti ya klabu hiyo kuwa asingependa kuzungumzia juu ya vurugu walizofanyiwa katika mchezo huo lakini ameelezea mchezo huo baada ya dakika 45 za kipindi cha kwanza huku akisema  timu yake ilionekana kutengeneza nafasi nyingi lakini ilishindwa kuzitumia kutokana na safu ya ushambuliaji  wake kutokuwa makini.

 

                                                                                                Picha na mtandao.

Pia  Cioaba amesema kwamba baada ya kuondolewa katika michuano hiyo sasa nguvu watazielekeza katika ligi kuu pamoja na kombe la  FA  kuwa moja ya mambo watakayoendelea kufanya ni kuhahakisha wanakusanya pointi za kutosha kwenye ligi na kutinga hatua ya fainali ya Kombe la FA ikiwemo kutwaa taji hilo .

 

Wakati ikiwa imebakisha mechi sita kuweza kumaliza ligi, Azam FC imefikisha alama 44 katika msimamo wa ligi na inashika nafasi ya tatu, ikizidiwa pointi 11 na kinara wa ligikuu  Simba anayeongoza, Yanga ni ya pili ikiwa imejizolea 53.

TOA MAONI YAKO HAPA