Na:Ayoub Mwigune

Ligi daraja la nne manispaa ya morogoro iliendelea tena hapo jana ambapo klabu ya mkundi united ilikuwa ikipambana dhidi ya  compassion mabapo  dakika 90 ziliweza kukamilika kwa sare ya 1-1 ambapo goli kwa upande wa mkundi lilifungwa na MARTIN ALOYCE  wakati kwa upande wa compassion goli lilikuwa la kujifunga kutokana na uzembe wa beki.

 

Ligi hiyo inatarajia kuendelea leo ambapo klabu SULTAN RANGERS itakuwa ikivaana na klabu ya MORO CITY huku zote zikiwa na alama saba katika kundi lao hivyo kufanya mchezo kuwa mgumu zaidi katika uwanja wa sabasaba katika manispaa ya morogoro.

 

                                                                                                             Picha na mtandao. 

 

Siku ya ya ijumaa wiki hii kutakuwa na mechi kati ya BEACH Boys ambao watacheza dhidi HOT STAR  katika kombe la PASAKA CUP ambalo lengo lake ni kuzipa changamoto timu za manispaa ya morogoro.

TOA MAONI YAKO HAPA