Na:Adam   Ramadhan

Katibu  mkuu   wa  baraza  la   wazee  katika  klabu  ya   Yanga  Ibrahimu   Akilimali  ametangaza  kuwania   nafasi  uenyekiti  iliyoachwa   wazi   siku  za  hivi  karibuni   na   aliyekuwa   Mwenyekiti   wa   klabu   hiyo  Yusuph   Manji.

Mzee  Akilimali   amesema   kuwa   amefikia  uamuzi    huo  ili  aweze  kuleta  mabadiliko  makubwa   zaidi  akitumia  busara  zake  licha  ya  kwamba   yeye   hana utajiri wa ki billionea   kama   alivyokuwa  Yusuph   Manji   kwa  wanajangwani   hao.

 

Picha na mtandao.

 

Akilimali   amedai  kuwa   anauwezo   mkubwa  wa  kuipa   Yanga  mafanikio katika   msimu  ujao   wa  soka  kwa  hivyo   anasubiri   uchaguzi  ujao  aweze  kugombea   huku  akiwa  na  imani  kubwa  ya kushinda  nafasi  hiyo kutokana na nafasi   kubwa   aliyonayo   katika   klabuu  hiyo.

TOA MAONI YAKO HAPA