MAYANGA ATANGAZA KIKOSI STARS

Na:Alfred Lukonge

Kikosi cha timu ya mpira wa miguu cha Tanzania 'Taifa Stars', kimesafiri kwenda jijini Mwanza kikiwa na ongezeko la wachezaji wapya saba.

Kati ya hao ambao Kocha Mkuu Salum Mayanga amewaita, wamo wale aliowatangaza juma lililopita ambao ni John Bocco, Kevin Sabato pamoja na kinda Athanas Mdamu ambaye anacheza Alliance ya Mwanza inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza.

Image result for Mayanga

Picha na mtandao.

 

Katika kikosi chake kabla ya kuivaa Rwanda Jumamosi ijayo, wachezaji wengine ambao Kocha Mayanga amewatangaza ni pamoja na Kipa wa Serengeti Boys - timu ya taifa a vijana ya Tanzania, Ramadhan Kabwili.

TOA MAONI YAKO HAPA