jinsi ya kuandaa mbegu ya uyoga

              

1.       Unatakiwa kuwa na chumba maalumu kisichopitisha mwanga

2.      Unatakiwa kuwa na presure cooker au jiko maalumu lenye moto mkali.

3.      Vyombo vya kuwekea mbegu kama vile glass, maji salama, ungaunga wa viazi vitamu, uteute unaotokana na mchemsho wa viazi vitamu pamoja na kibakuli kidogo chenye mfuniko.

4.      Kipande cha uyoga ambacho kitachanganywa na maji salama, ungaunga wa viazi vitamu, uteute unaotokana na mchemsho wa viazi vitamu,  kwa ajili ya kutengeneza fangasi ambao watatumika kutengeneza mbegu ya uyoga.

5.      Baada ya  kuchanganya  mchangnyiko huo, chemsha mchanganyiko huo kwenye presha cooker au jiko la moto mkali.

6.      Ipua na weka mchanganyiko huo kwenye vibakuli vidogo vinne vyenye mfuniko [4]

7.      Acha  upoe kwa dakika kumi na tano.

8.     Chukua vipande vya uyoga weka kwenye mchanganyiko  uliouweka kwenye bakuli ndogo yenye mfuniko  halafu funika na hifadhi sehemu yenye joto ili kukuza fangasi kwa muda wa siku kumi au kumi na tano.

9.      Baaada ya siku kumi na tano fangasi zitakuwa tayari kwa ajili ya kuendelea kuandaa mbegu ya uyoga.

10.  Hifadhi fangasi hao kwenye friji ili wasiendelee kukua.

 

Baada ya kuandaa fangasi hatua inayofuata ni;

 

 

1.        Andaa mtama kilo hamsini [ kg 50]

2.      Chemsha mtama  kwenye jiko lolote mpaka uive kwa kupasukapasuka

3.      Ipua na chuja maji

4.      Baada ya kuchuja weka mtama wako kwenye chupa au kopo lenye mfuniko,weka katika chupa nyingi  kadiri uwezavyo.

5.       Weka kwenye preasure cooker au jiko lenye moto mkali kwa muda wa saa moja

6.      Ipua na acha upoe

7.      Baada ya kupoa chukua fangasi katakata vipande vipande na kila  kipande weka kwenye kopo au chupa yenye mtama.

8.     Funika kwa muda wa siku kumi na tano mbegu itakuwa imekomaa na tayari kwa kupandwa katika shamba uliloliandaa..  

Aina ya mbegu tuliyoiandaa hapa ni mamama/ oista mashroom.. uyoga zao linalotumika kukuza uchumi kwa wakulima kwani linahitajika sana mahotelini kwa ajili ya supu. lakini uyoga huo pia unatumika majumbani kwa mlo ambao una lishe bora kwa familia.

 

NB; mahitaji yote unaweza kuyatengeneza ukiwa nyumbani au unaweza kuvipata kwa  kununua kwenye maduka kwa kutumia majina yafuatayo;

-           Agger- ungaunga wa viazi vitamu

-          Distil water-maji salama

-          Bikker –glass

-          Maltexxtract-uteute unaotokana na mchemsho wa viazi vitamu

-          Pret dish-kibakuli kidogo chenye mfuniko.

TOA MAONI YAKO HAPA