Bi Domina alisema  kutokana na takwimu za Wizara ya Afya imeonekana Tanzania inakabiliwa na tatizo la udumavu kwa 42% , ukondefu 5% udhoofu 16%  hii inatokana na watanzania wengi kutotumia vyakula vya kuongeza vitamin A kama viazi lishe

Aidha aliongeza kuwa viazi lishe vinafaida nyingi katika mwili wa binadamu vilevile husadia katika kuongeza kipato na kuinua uchumi wa kila mkulima hivyo kuwataka wakulima wasikidharau kilimo hicho na kuzidi kutumia fursa mbalimbali za kuendeleza kilimo hicho pindi zinapowafikia

Ameongezakuwa Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA  kimeweza kusambaza mbegu aina ya Kiegea, Naspot na Kabode katika vijiji mbalimbali vya Wilaya ya Mvome ro katika shule za msingi ili kurithisha elimu hiyo kwa wanafunzi ambao wataweza kuifikisha kwa wazazi wao na kuwahamasisha kulima kilimo hicho kwa lengo la kupunguza tatizo la ukosefuwa vitamin A kwa jamii.

Naye mmoja wa wazazi waliohudhuria katika shuguli hizo Bwana Mohamed Khamisi Mwasimba aliisifu timu nzima ya wawezeshaji kwa kuweza kufika katika Wilaya hiyo na kutoa ushuhuda juu ya mbegu waliyopewa kwa kilimo cha viazilishe ambacho kimeweza kuwaletea mafanikio

Bwana Mwasimba alisema hali ya sasa imekuwa nzuri maradufu ukilinganisha na mbegu waliyokuwa wakiitumia hapo awali kwani mbegu hiyo kutoka SUA imeonekana kuhimiri hata ukame

“nawashukuru sana wa tuwa SUA kwa kutuletea mbegu hii imeonekana ni nzuri inahimiri ukame hasa katika kipindi hiki hakuna mvua lakini ukiangalia mashambani viazi vimejaa tunafurahia kwakweli”alisema Mwasimba

Mradi huo unaotekelezwa na Dr Gratian Lwegasira chini ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) unatekelezwa kwa miaka mitatu kuanzia 2015 hadi 2018  ambapo mpaka sasa umeweza kuongeza idadi ya wakulima waviazilishe katika wilaya ya Mvomero na kuonekana ni zao lenye tija kwakuwaongeza kipato cha wakulima.