Picha na mtandao       

Na: Tatyana Celestine

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, SUA, kupitia kituo cha Utafiti wa Ufuatiliaji wa Magonjwa Ambukizi cha kusini mwa Afrika, SACIDS, kimepokea ombi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo DRC, kutuma timu ya wataalamu kwenda kusaidia kukabili ugonjwa wa Ebola uliozuka nchini humo hivi karibuni.

Hayo yameelezwa na Mtafiti kiongozi kutoka SUA, Prof Ezron Karimuribo alipokuwa akijibu swali kuhusu nafasi ya  mpango-maombi wa Data-Afya kukabiliana na hatari ya ugonjwa wa Ebola uliozuka huko DRC, usiingie nchini na kuhatarisha afya za watanzania.

Bofya hapa kwa Habari zaidi.....

Picha na Tatyana Celestine   

Na: Bujaga I. Kadago

Wakurugenzi wa halmashauri nchini wametakiwa kuwatumia wataalamu kutoka kituo cha Utafiti na Ufuatiliaji wa magonjwa ambukizi cha kusini mwa Afrika SACIDS- SUA, ili waweze kunufaika na faida za kupata taarifa kuhusu majanga mbalimbali lakini pia kupata taarifa nyingine zaidi ya zile za majanga pekee.

Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi wa kuratibu na kukuza Utafiti katika Taasisi ya Taifa ya magonjwa ya Binadamu, NIMR, Dr. Paul Kazyoba alipokuwa akitoa neno la shukrani wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mpango-Maombi (APP) wa Afya-Data hafla iliyofanyika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, SUA, mjini Morogoro.

Bofya hapa kwa Habari zaidi.....

  Picha na Tatyana Celestine   

Na: Bujaga I. Kadago

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, SUA, kimewataka wadau katika sekta za afya ya binadamu, wanyama na mimea kuanza sasa kutumia mpango maombi yaani APP ya afya data ili kukabili mlipuko wa magonjwa kwa haraka  kupitia taarifa sahihi za picha za eneo husika. 

 

Kauli hiyo imetolewa na Makamu Mkuu wa chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo, SUA, Prof. Raphael Chibunda alipokuwa akizindua rasmi Mpango Maombi wa Afya Data chuoni SUA kufuatia kukamilika kwa utafiti na majaribio yaliyofanywa na kituo cha umahiri  kituo cha utafiti na Ufuatiliaji wa magonjwa ambukizi kusini mwa bara la Afrika SACIDS  kwa kushirikiaa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa magonjwa NIMR.

Bofya hapa kwa Habari zaidi.....

Subcategories

TOA MAONI YAKO HAPA