Na:Alfred Lukonge

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. DKT. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Florens D.A.M Luoga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA).

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Gerson Msigwa, Prof. Luoga anachukua nafasi ya Bw. Benard Mchomvu ambaye bodi yake ilivunjwa na uteuzi wake kutenguliwa.

Image result for prof florens luoga

Picha na mtandao

 

Prof. Luoga ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Dar es Salaam upande wa taaluma na uteuzi wake unaanza kazi mara moja.

TOA MAONI YAKO HAPA