Na:Mwandishi Wetu

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki amesema Watumishi wa  Umma walioghushi vyeti watachukuliwa hatua za kisheria.

Mhe. Kairuki ameyasema hayo katika kikao kazi na watumishi na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Temeke,Tarafa ya Mbagala na kusisitiza kuwa wote  walioghushi vyeti hawapo kazini na wameshafutwa katika orodha ya malipo ya Serikali.

Image result for KAIRUKI                                                                                                                                    Picha na mtandao.

 

Akiongelea watumishi wa umma walioajiriwa na sifa za darasa la saba Mhe. Kairuki amesema kuwa, endapo mtumishi aliajiriwa kabla ya tarehe 20 Mei 2004 anastahili kuendelea kuwa katika Utumishi wa Umma, na endapo kajiendeleza abadilishiwe muundo kuendana na sifa za elimu aliyopata, lakini endapo mtumishi aliajiriwa baada ya tarehe 20 Mei 2004 anatakiwa kuwa na sifa ya elimu ya kidato cha nne.

 

TOA MAONI YAKO HAPA