Na:Alfred Lukonge

 Imeelezwa kuwa sera ya ugani inayoendelea kufanyiwa marekebisho katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA ) imelenga kuhakikisha teknolojia mbalimbali zinazopatikana chuoni humo zinawafikia wakulima hasa wale wadogo ili waweze  kulima kilimo chenye tija.

Hayo yamebainishwa na Dk. Innocent Babili kutoka Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza (I.C.E) chuoni SUA kwenye mkutano uliojikita kujadili sera ya ugani ya chuo hicho ( OUTREACH POLICY), mkutano uliojumuisha wajumbe kutoka kila idara chuoni humo.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

                                        

Na: Calvin Gwabara

Wakazi wa wilaya ya Buchosa Mkoani Mwanza wameiomba Serikali na watafiti kuharakisha upatikanaji wa mbegu bora ya mahindi ambayo hayashambuliwi na mdudu maarufu kama Bungua ambaye hushusha uzalishaji.

Wakiongea na SUAMEDIA katika soko la wilayani hapo wamesema kwa muda mrefu sasa zao la mahindi limekuwa likikabiliwa na tatizo la funza hao ambao wamekuwa wakishambulia mahindi na hivyo kupelekea mavuno madogo na wakati mwingine mkulima kushindwa kuzalisha.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

                                   

Na:Gerald Lwomile

Chuo Kikuu cha Sokoine cha  Kilimo SUA, kimetajwa kama chuo chenye hadhi ya kimataifa, ambacho mwanafunzi anyehitimu katika Chuo hicho anaweza kwenda kusoma katika Chuo chochote Duniani.

Hayo yamesemwa na Makamu wa Mkuu wa Chuo hicho Prof Raphael Chibunda katika siku maalumu ya ufunguzi wa kuyajua mazingira ya chuo, ikiwa ni pamoja na kujua sheria na taratibu za chuo  maarufu kama "Orientation week".

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

Subcategories

TOA MAONI YAKO HAPA