Image result for sokoine university administration building                           

Na:Farida Mkongwe

Wanafunzi wapya wanaojiunga na masomo kwa mwaka wa masomo 2017/2018 katika Chuo Kikuu cha Sokine cha Kilimo SUA wametakiwa kuhakikisha wanashiriki kwenye wiki ya maelekezo ya mazingira na taratibu za chuo “Orientation week” ambayo inatoa nafasi kwa wanafunzi hao kujua muundo wa chuo pamoja na kukutana na viongozi mbalimbali waliopo chuoni hapo.

Wito huo umetolewa na Naibu Makamu wa Mkuu wa Chuo Taaluma Prof. PETER GILLAH wakati akizungumza na SUAMEDIA ofisini kwake kuhusu manufaa ya wiki hiyo kwa wanafunzi wapya ambapo  shughuli mbalimbali hufanyika ikiwa ni pamoja na kupata maelekezo ya namna ya kuishi chuoni hapo .

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

                                            

Na:Alfred Lukonge

Mwenyekiti wa kamati ya shule ya msingi Makuyu Bw.Omari Issa iliyopo wilayani Mvomero mkoani Morogoro amesikitishwa na dhana iliyojengeka miongoni mwa watanzania kuwa kila kitu wanachohamasishwa kuchangia uhishia mikononi mwa wajanja wachache, jambo ambalo linachangia kudidimiza maendeleo ya shule hiyo.

Bw.Issa amebainisha hayo alipozungumza na SUAMEDIA mjini Morogoro hivi karibuni na kusema kuwa mpango wa elimu bure wananchi wengi wameshindwa kuuelewa, hasa kwenye suala la uchangiaji wa chakula na kuboresha miundombinu, hivyo pindi kamati yake inapohamasisha wananchi washiriki kwenye kuchangia chochote  huonekana wanataka kuwaibia.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

                         

Na:Calvin Gwabara

Mkuu wa mkoa wa Mara Adamu Malima amewataka watendaji wa umma kubadili kilimo toka cha mazoea kwenda kilimo cha utafiti ili kuwawezesha wakulima kupata mazao mengi katika msimu huu.

Akizungunza na watendaji na viongozi wa madhehebu ya dini na vyama vya siasa mkuu huyo wa mkoa amesema hayo  wakati alipokuwa akijitanbulisha rasmi kwao ikiwa ni siku ya pili kuanza kazi katika mkoa huo.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

Subcategories

TOA MAONI YAKO HAPA