Na: Calvin  Gwabara

Wananchi wilayani Chato Mkoani Geita wameishukuru tume ya taifa ya sayansi na teknolojia COSTECH kwa kuwawezesha kupata mbegu bora za viazi lishe aina ya Kabodee ambavyo vitasaidia kumaliza matatizo ya ukosefu wa vitamin A kwa watoto, wazee na jamii kwa ujumla.

Kauli hiyo ya pamoja imetolewa na wanakikundi wa Muungano kwenye kata ya Kigongo wilayani chato wakati wakikabidhiwa mbegu hizo kuzipanda kwenye shamba darasa ili kupata mbegu za kusambaza kwa wakulima wengine.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

 

                             

Na:Alfred Lukonge

Utafiti umebaini asilimia 90 ya bajeti inayotengwa kwenye sekta ya elimu hutumika kulipa mishahara ya watumishi wa kada hiyo na kuacha changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo.

Hayo yamesemwa Bw.Zolote Loilang’akaki mwenyezeshaji kutoka Mtandao wa Elimu Tanzania (TenMet) alipokuwa anawasilisha matokeo ya utafiti uliofanyika kwenye baadhi ya shule za msingi na sekondari wilayani Mvomero mkoani Morogoro kuangalia jinsi bajeti zinavyoandaliwa na matumizi yake.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

                           

Na:Halima Katala Mbozi

Wafanyabiashara wadogo wa chumvi  halmashauri ya Kilwa  Masoko mkoani Lindi wamelalamikia kushuka kwa bei ya chumvi ambayo imekuwa changamoto kubwa kwa wafanyabiashara hao.

Akizungumza na wanahabari wakati wa ziara ya kutembelea na kujionea shughuli za kimaendeleo kwa mji huo Bi. Amina Juma ambaye ni mwenyekiti wa kikundi cha wanawake  cha TUJIKOMBOE kilichopo mtaa  wa Jangwani halmashauri ya Kilwa Masoko amesema kuwa katika uvunaji wa chumvi kuna changamoto kubwa ikiwemo ya soko ambalo kwa sasa lipo chini kiasi cha kutaka kuwakatisha tamaa.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

Subcategories

TOA MAONI YAKO HAPA