Na:Alfred Lukonge

Hamasa imetolewa kwa vijana wasio na ajira hapa nchini kuweka juhudi kwenye shughuli ndogondogo za uzalishaji mali pamoja na kuwa wabunifu wa vitu mbalimbali kama njia mojawapo ya kukabiliana na tatizo la ajira hapa nchini.

Hamasa hiyo imetolewa na Bw. Emmanuel Gasper ambaye ni mwezeshaji kutoka Shirika lisilo la kiserikali la Trainning For Life alipozungumza na SUAMEDIA mapema hii leo kutoka mkoani Kilimanjaro.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

                             

Na:Amina Hezron

Wito umetolewa kwa waendesha mitandao katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kuitumia mitandao ya kijamii ipasavyo kwa kufikisha taarifa mbalimbali zinazohusu  chuo, kwani mitandao hiyo kwa sasa watu wengi hufanya mawasiliano kupitia mitandao hiyo.  

Wito huo umetolewa na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma Prof. Peter Gillah katika kikao cha robo ya nne ya mwaka cha kamati ya tovuti ya chuo na kubainisha kuwa dunia hivi sasa  imebadilika kwani taarifa   zote zinapatikana kiganjani, hivyo jitihada za dhati zinahitajika kufanyika kupitia mitandao ya kijamii kwenye katika kufikisha  taarifa za chuo ili zipate mashiko zaidi.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........


 

                                                             

Na:Calvin Gwabara

Watanzania hususani wafanyakazi wametakiwa kuunga Mkono jitihada za Serikali ya awamu ya tano kwa vitendo ili kusaidia kuondoa umasikini kwa wananchi hususani kupitia miradi mbalimbali ya kilimo.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa wilaya ya Kyerwa Mkoani Kagera Mhe. Kanali mstaafu Shaban Lissu wakati akizungumza na wakulima wakati wa uzindua wa mbegu bora za Migomba iliyozalishwa kwa njia ya chupa kwaajili ya shamba darasa kwa wakulima katika kijiji cha Mulutunguru  wilaya ya Kyerwa iliyofadhiliwa na Tume ya taifa ya sayansi na teknolojia (COSTECH) kupitia Jukwaa la bioteknolojia kwa maendeleo ya kilimo Tanzania (OFAB).

Bofya hapa kwa Habari zaidi.....

 

Subcategories

TOA MAONI YAKO HAPA