Na:Gerald Lwomile

Serikali  imekubali ombi la Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA la kusaidia ujenzi wa maabara katika kituo cha utafiti  Ndaki ya Tiba ya Wanyama  na Sayansi za Afya ili kukabiliana na magonjwa yanayoambukiza kwa wanyama na binadamu.

Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya utafiti wa vyura wa Kihansi, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mh. Kangi Lugola amesema moja ya kazi kubwa ya Serikali ni kuzipatia ufumbuzi chamgamoto mbalimbali hivyo ameiagiza NEMC kusaidia ujenzi huo.

Bofya hapa kwa Habari zaidi.....

 

                                          

Na: Farida Mkongwe

Abiria wanaosafiri na mabasi mbalimbali wametakiwa kupaza sauti na kutoa ushirikiano wa kina kwa jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani kuhusu madereva wanaokiuka sheria ili kupunguza na hatimaye kuondoa kabisa ajali za barabarani zinazoweza kuepukika.

Wito huo umetolewa na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi ambaye pia ni Mkaguzi wa Magari na Mtahini wa Madereva mkoa wa Morogoro Yusuph Ali Masoli wakati akizungumza na SUAFM kuhusu njia mbalimbali za kuepukana na ajali za barabarani pamoja na ukaguzi unaofanyika katika kipindi hiki cha maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani.

Bofya hapa kwa Habari zaidi.....

 

 

   

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kimesaini mkataba na Kampuni ya Mawasiliano Tanzania TTCL ya kutoa huduma ya mtandao wa “internet” wenye kasi na uhakika kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya chuo.

Akizungumza wakati wa utiaji saini wa makubaliano hayo Makamu Mkuu wa Chuo  cha SUA Prof. Raphael Chibunda amesema huduma za mtandao chuoni hapo ni muhimu kwa shughuli mbalimbali za chuo na pale huduma hizo zinapokosekana huathiri utekelezaji wa majukumu ya chuo kwa kiwango kikubwa

Bofya hapa kwa Habari zaidi.....

 

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Save

Subcategories

TOA MAONI YAKO HAPA