Benki ya CRDB imetangaza bidhaa yao mpya iitwayo “Salary Advance” kwa Watumishi wa umma ambapo ilifanya mkutano wake na Menejimenti ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo siku ya Jumatatu tarehe 09/10/2017.

Mwenyekiti wa Mkutano huo Prof. Y.M. Ngaga, Naibu Makamu wa Mkuu wa Chuo (Utawala na Fedha ) alifungua mkutano huo kwa kumtambulisha Kiongozi wa msafara wa Menejimenti ya Benki  Bi. Grace Maseki, Meneja wa Benki ya CRDB tawi la SUA ambaye aliongozana na Viongozi mbalimbali kutoka Makao makuu ya Benki ya CRDB.

 Bofya hapa kwa Habari zaidi.....

                    

Na:Alfred Lukonge

 Mkurugenzi wa Taasisi ya Mkulimastar Bw. Egno Gerald Ndunguru amesema kuwa mkulima akiwa na maarifa mazuri ya kilimo yatamsadia kupata matokeo bora hivyo ni muhimu  kuwa na elimu ya kitu chochote anachotaka kukifanya.

Ndunguru amesema hayo hivi karibuni alipozungumza na SUAMEDIA na kubainisha kuwa wakulima wengi wanafeli kufanya kilimo chenye tija kwa kukosa maarifa, na kwamba Taasisi yake imejipanga kuhakikisha inatoa elimu stahiki kwa wakulima  hapa nchini ili waweze kupata matokeo bora.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

                      

Na:Mwandishi Wetu

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ambaye pia ni kamishna mstaafu wa Jeshi la Polisi Zelote Steven  amekutana na uongozi wa Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania – TAWA na kuuomba uongozi huo  kusaidia operesheni za kuondoa mifugo katika wilaya zote za Mkoa wake.

Mkuu huyo  wa Mkoa pamoja na kusifu juhudi zinazofanywa na askari wanyamapori kutoka mapori ya Akiba ya  Uwanda na Lwafi Mkoani Rukwa katika kutekeleza majukumu yao, pia amewataka askari hao  kuangalia uwezekanao wa suala la kuondoa ng'ombe Ndani Ya hifadhi ambapo hadi sasa . ng'ombe 319 wamekamatwa ndani. ya pori la Akiba Uwanda.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

Subcategories

TOA MAONI YAKO HAPA