Na:Alfred Lukonge

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA)  upande wa taaluma Prof.Peter Gillah amesema kuwa baraza la wafanyakazi lengo lake kuu sio kufanya vita na utawala bali ni kiunganishi kizuri cha kupeleka maslahi ya wafanyakazi katika uongozi wa juu ili yaweze kufanyiwa kazi.

Prof.Gillah amesema hayo mapema hii leo alipokuwa anafungua semina kwa wajumbe wapya na wale wanaoendelea wa baraza kuu la wafanyakazi chuoni SUA kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo na kubainisha kuwa kupitia semina hiyo wajumbe watapata njia bora za kufanya kazi kwa maendeleo ya chuo.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

                        

Na:Vedasto George

Wakulima  wametakiwa kufuata kanuni bora za kilimo pamoja na kuwatumia wataalam wa kilimo wanaopatikana nchini ili kuondokana na changamoto zinazowakabili ikiwemo  ile ya  magonjwa yanayoathiri mazao.

Wito huo umetolewa na  waziri wa kilimo Mhe. Charles Tizeba wakati akisoma hotuba kwa niaba ya Waziri Mkuu Mhe. Kasim Majaliwa  kwenye warsha ya  siku mbili ya mkutano mkuu wa  22 wa  Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania ( MVIWATA).

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Jaji Joseph Warioba aliyevaa suti nyeusi akiwa tayari kusimikwa katika mahafali ya 33 ya chuo hicho

 

 

Na Gerald Lwomile

 

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Jaji mstaafu Joseph Sinde Warioba amesimikwa rasmi kuwa Mkuu wa Chuo hicho katika mahafali ya 33 iliyofanyika novemba 24 2017.

 

Jaji Warioba ambaye aliteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungao wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli amechukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Chuo hicho Anur Kasssam.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

Subcategories

TOA MAONI YAKO HAPA