Na:Alfred Lukonge

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo mkoni Morogoro SUA kimepongezwa kwa namna kinavyotengeneza ajira binafsi kwa wahitimu wake kwa kuwapatia mafunzo mbalimbali ya kuongeza thamani mazao ya kilimo kupitia Shirika la wajasiliamali  wanafunzi waliohitimu chuoni humo  (SUGECO)

Pongezi hizo zimetolewa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Hamisi Ulega kwenye sherehe za 23 za majalisi chuoni hapo ambapo  alimuwakilisha waziri wa wizara hiyo.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

                         

Na:Calvin Edward Gwabara

Mkurugezni wa Taasisi ya elimu ya kujiendeleza ICE iliyopo katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA,  Prof. Caroline Nombo amewaomba wajumbe wa bodi ya ICE kuhakikisha wanaisaidia Taasisi hiyo kutekeleza majukumu yake kwa kuifikisha SUA kwa jamii na wadau wote lengwa wa kazi za chuo.

Ombi hilo amelitoa wakati akizungumza na wajumbe wa bodi hiyo wakati wa kikao cha bodi ambacho pia kiliwakutanisha wajumbe wapya wa bodi kutoka nje ya SUA ambao ni Bwana Francis Sabuni kutoka Mfuko wa Uhifadhi wa Milima ya Tao la Mashariki pamoja na Dkt. Erenest Mwasalwiba kutoka Chuo Kikuu Mzumbe.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

                                 

Na:Alfred Lukonge

Rais wa serikali ya wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Bw.Peter Laurent Magembe amesema kuwa lengo kuu la Taasisi hiyo ni kuwa daraja kati ya wanafunzi na menejimenti ya chuo hicho kwenye kuwasilisha maslahi yao.

Bw.Magembe ambaye Taasisi hiyo anayoiongoza hujilikana kwa jina la  Sua Student’s Organization (SUASO) amesema hayo kwenye kipindi cha Tanzanite kinachorushwa hewani na redio SUA FM ambapo aliambatana  na makamu wake Bw.Malima Daniel.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

Subcategories

TOA MAONI YAKO HAPA