LATEST NEWS

Njia za kukabiliana na maoni mabaya juu ya kazi yako

Njia za kukabiliana na maoni mabaya juu ya kazi yako

13 December 2018
Maoni ni sehemu muhimu ya ukuaji wa kazi zako kitaaluma. Huonyesha ikiwa utendaji wako ni mzuri au mbaya na ni maeneo gani unapaswa kuboresha. Kupokea maoni hasi kazini inaweza kuwa ni kitu kigumu kusikia, lakini ni fursa ya kujifunza na kutumia somo...
Readmore
MAMBO 6 MUHIMU YA KUFANYA KABLA YA KUSTAAFU

MAMBO 6 MUHIMU YA KUFANYA KABLA YA KUSTAAFU

07 December 2018
Kustaafu ni msimu mpya ambao kila mwajiriwa anapaswa kuufahamu na kujiandaa kwa msimu huo vyema. Kumeshuhudiwa watu wakiishi maisha ya taabu na mahangaiko makubwa baada ya kustaafu. Hili linatokana na kutokujiandaa vyema kabla ya kustaafu. Kwa kufaha...
Readmore
Mahafali ya 34 SUA

Mahafali ya 34 SUA

25 November 2018
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA, Jaji mstaafu Joseph Sinde Warioba ametunuku Shahada mbalimbali kwa wahitimu 2695 huku zaidi ya wahitimu 50 wakipata shahada ya Udaktari wa Falsafa katika Fani mbalimbali.     Mkuu huyo wa Chuo...
Readmore
MKOJO WA PAKA UNAVYOWANUFAISHA WAKULIMA

MKOJO WA PAKA UNAVYOWANUFAISHA WAKULIMA

16 November 2018
Na Farida Mkongwe  Viongozi na Wakulima wa kijiji cha Mikese wamekishukuru Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kwa kufanya utafiti uliobaini kuwa mkojo wa paka unaweza kufukuza panya wa mashambani na majumbani ambao kwa kiasi kikubwa wamekuwa...
Readmore
Wizara ya Madini haitawavumilia watendaji wanaokuwa  chanzo cha upotevu wa maduhuli

Wizara ya Madini haitawavumilia watendaji wanaokuwa  chanzo cha upotevu wa maduhuli

15 November 2018
Na:Gerald Lwomile Wizara ya Madini imesema haitawavumilia watendaji wanaokuwa  chanzo cha upotevu wa maduhuli katika wizara hiyo na kuahidi kutoa msaada wa kila hali katika kuhakikisha watendaji hao wanakusanya maduhuli hayo na kufikia malengo....
Readmore

SEHEMU YA 4: UFUGAJI WA SAMAKI HATUA KWA HATUA

                               HATUA YA 2: UCHIMBAJI WA BWAWA

Katika sehemu hii ya 4 tunaangalia hatua ya 2 ambayo ni uchimbaji wa bwawa. Jambo la kwanza la kuangalia ni vipimo. Kimsingi kwa mujibu wa Mhadhiri Mwandamizi katika Idara ya Sayansi ya Wanyama iliyopo Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Dr. Berno Mnembuka ambaye pia ni mtaalamu wa lishe ya samaki na uzalishaji hakuna vipimo maalum vya ukubwa wa bwawa maana ukubwa wa bwawa unategemea eneo na malengo. Kwa mfanyabiashara bwawa kubwa litakuwa ni bora zaidi kwake ili aweze kuvuna samaki wengi zaidi ukilinganisha na mtu anayefuga kwa ajili ya chakula.

Jambo la pili ni kuwa unapochimba bwawa unatakiwa kuchimba upande mmoja uwe na kina au umbali wa  mita 1.5 (mita moja na nusu) na upande mwingine mita 1 na sentimita 20 kwenda chini. Hii ni kwa sababu mianya ya jua ambayo inapeleka mwanga ardhini haiwezi kupenya kwenda chini zaidi ya mita 1.5 na hivyo ukizidisha zaidi ya hapo utakuwa umepoteza nguvu zako bure na ukipunguza utakuwa umeathiri ustawi wa samaki.

Mtaalamu huyu wa lishe ya samaki na uzalishaji Dr. Mnembuka anasema kuwa umbo la bwawa la kufugia samaki ni vizuri likawa la mstatiri ili kurahisisha shughuli za uvunaji kwa kuwa hata wavu utakaotumika kuvunia na idadi ya watu watakaohitajika katika shughuli za uvunaji watakuwa ni wachache ukilinganisha na maumbo mengine,  pia kama unatumia mashine umbo la mstatiri ni zuri zaidi kwa sababu hata gharama yake ya uchimbaji inakuwa ni ndogo tofauti na maumbo mengine.

Sambamba na hilo katika uchimbaji kitako cha bwawa hakitakiwi kiwe tambarare kinapaswa kiwe na mwinuko upande mmoja ili kukusaidia kuweza kutoa maji kwa urahisi pale unapokuwa huyahitaji.

Vile vile kingo za bwawa zinatakiwa ziwe zimechongwa kuegemea nje ili kukinga bwawa lisibomoke wakati wa kujaza maji. Pia iwapo kingo hizo za bwawa zitakuwa zimechongwa kuegemea nje itakusaidia uweze kuingia bwawani kwa urahisi tofauti na kingo zikiwa zimesimama.

Bwawa linaweza kuchimbwa kwa mikono au kwa mashine, njia hizo zote mbili ni sahihi isipokuwa kama bwawa ni kubwa au kama unakusudia kufuga kibiashara ni vema ukatumia mashine kwa sababu mashine inafanya kazi kwa haraka na hivyo kumaliza mapema, pia ufanisi wake unakuwa ni mkubwa ukilinganisha na ufanisi wa bwawa linalochimbwa kwa mikono.

Kwa kuhitimisha hatua hii ya 2 ya uchimbaji wa bwawa la kufugia samaki inasisitizwa kuwa ni vizuri ukazingatia maelezo ya kitaalamu katika uchimbaji wa bwawa ili uweze kufanikiwa katika  kazi hii ya ufugaji wa samaki.

Usikose kufuatilia sehemu ya 4 ambayo itakuwa ikizungumzia hatua ya 3 ya ufugaji wa samaki ambayo ni uandaaji na upandikizaji wa vifaranga au mbegu za samaki katika bwawa lako.

 

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner