LATEST NEWS

Kituo cha Utafiti wa kilimo cha Mlingano kwa kushirikiana na wadau wengine wameanza utafiti wa kuwezesha zao la mkonge kuzalisha Mvinyo

Kituo cha Utafiti wa kilimo cha Mlingano kwa kushirikiana na wadau wengine wameanza utafiti wa kuwezesha zao la mkonge kuzalisha Mvinyo

18 September 2019
Kituo cha Utafiti wa kilimo cha Mlingano kwa kushirikiana na wadau wengine wa ndani na nje ya Tanzania wameanza utafiti wa kuwezesha zao la mkonge kutoa bidhaa ya Mvinyo katika zao la mkonge kutokana  na Tanzania kupata nyuzi pekee ambayo ni sa...
Readmore

KAMA UNATAKA KUENDELEZA KIPAJI USIOGOPE KUJARIBU- FASHION

Na: ALFRED LUKONGE                                      

 

Imeelezwa kuwa kama msanii ana kipaji hata siku moja asiogope kujaribu pamoja na kutokata tamaa kama kweli anataka kuendeleza kipaji chake

Hayo yamesemwa na msanii chipukizi wa muziki wa kizazi kipya kutoka mji wa Morogoro Ramadhani Mashaka maarufu kama “Fashion” alipozungumza na SUAMEDIA na kubainisha kuwa “ muziki sasa hivi ni ajira hivyo kama mtu ameamua kuufanya ahakikishe  ameweka malengo muziki  kuvuka mipaka ya Tanzania”.

Pamoja na hayo Mashaka ametoa wito kwa wasanii wachanga kutafuta ushauri kwa watu wenye weledi na muziki ili kupata mbinu ni namna  gani wanaweza kupenya kwenye soko la kimataifa.

Akizungumzia singo yake mpya aliyotoa hivi karibuni inayokwenda kwa jina “ Vumilia” Mashaka amesema wimbo huo ni kisa cha kweli kilichomkuta rafiki yake wa karibu aliyekuwa anatoka kijijini kwenda mjini kutafuta maisha na kumuasa mpenzi wake avumilie mpaka atakaporudi.

Pia msanii huyo alibainisha baadhi ya changamoto zinazomkabili ni ukosefu wa fedha za kurekodia nyimbo zake kwani anazo nyimbo nyingi pamoja na kutopata ushirikiano wa kutosha kutoka kwenye vyombo vya habari.

Msanii Mashaka alianza kujishughulisha na muziki mwaka 2009 kipindi hicho akiwa  darasa la sita katika kijiji cha Lusanga tarafa ya Turiani wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro na msanii anayemvutia ni Belle 9.

 

 

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner