LATEST NEWS

Kituo cha Utafiti wa kilimo cha Mlingano kwa kushirikiana na wadau wengine wameanza utafiti wa kuwezesha zao la mkonge kuzalisha Mvinyo

Kituo cha Utafiti wa kilimo cha Mlingano kwa kushirikiana na wadau wengine wameanza utafiti wa kuwezesha zao la mkonge kuzalisha Mvinyo

18 September 2019
Kituo cha Utafiti wa kilimo cha Mlingano kwa kushirikiana na wadau wengine wa ndani na nje ya Tanzania wameanza utafiti wa kuwezesha zao la mkonge kutoa bidhaa ya Mvinyo katika zao la mkonge kutokana  na Tanzania kupata nyuzi pekee ambayo ni sa...
Readmore

WASANII WATAKIWA KUACHA   KUAMINI KUWA  KAZI NZURI LAZIMA IFANYIKE STUDIO FULANI

Na: ALFRED LUKONGE

Wasanii chipukizi katika mji wa Morogoro wametakiwa kuacha kasumba mbaya iliyojengeka miongoni mwao ya kuamini kuwa ili utoe kazi nzuri ni lazima uende kwenye studio fulani kwani kazi nzuri inaweza kutoka sehemu yoyote.

Hayo yamesemwa na mtayarishaji wa muziki kutoka studio ya Uptown Music iliyoko mjini Morogoro Jonathan Kutona maarufu kama “King niva” alipofanya mahojiano na SUAMEDIA Jumamosi ya Machi 26 na kubainisha kuwa “ kama mtu ana kipaji anaweza kutengeneza wimbo wake katika studio yoyote na  watu wakamwelewa”.

Pia mtayarishaji huyo aliwaasa wasanii kutafuta kazi za kuwaingizia kipato huku wakifanya muziki kwani muziki ni biashara yenye mlolongo mrefu hadi ufahamike, hivyo msanii anatakiwa awe na kitu cha kufanya ili kuondokana na tabia ya wasanii kuwa ombaomba.

Akizungumzia safari yake ya utayarishaji muziki Kutona amebainisha kuwa alianza kwa kununua programu mbalimbali za kutengeneza midundo na kuanza kutayarisha midundo bila mpangilio hadi ilipofika mwaka 2012 alipokutana na Dupah na kuanza kumpa darasa la utayarishaji wa muziki pamoja na mafunzo mbalimbali yanayopatikana kupitia mtandao.

Kutona ametoa wito kwa wasanii wa Morogoro kujiamini kwani kila mwimbaji ana kitu  cha kipekee alichopewa na mwenyezi Mungu. Pamoja na hayo mtayarishaji huyo ameomba   sapoti kutoka vyombo vya habari hasa vya mjini Morogoro ili wasanii wa mji huo waweze kufahamika.

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner