LATEST NEWS

Kituo cha Utafiti wa kilimo cha Mlingano kwa kushirikiana na wadau wengine wameanza utafiti wa kuwezesha zao la mkonge kuzalisha Mvinyo

Kituo cha Utafiti wa kilimo cha Mlingano kwa kushirikiana na wadau wengine wameanza utafiti wa kuwezesha zao la mkonge kuzalisha Mvinyo

18 September 2019
Kituo cha Utafiti wa kilimo cha Mlingano kwa kushirikiana na wadau wengine wa ndani na nje ya Tanzania wameanza utafiti wa kuwezesha zao la mkonge kutoa bidhaa ya Mvinyo katika zao la mkonge kutokana  na Tanzania kupata nyuzi pekee ambayo ni sa...
Readmore

ILI KUSHINDA MAJARIBU WANADAMU AWANA BUDI KUMTAFUTA MUNGU KWA JUHUDI ZOTE

Na: ALFRED LUKONGE

Imeelezwa kuwa wanadamu awana budi kumtafuta Mungu kwa juhudi zote ili waweze kuyashinda majaribu yote ya dunia kama kweli wanataka kuuona ufalme wa mbingu.

Hayo yamesemwa na mwanamuziki wa nyimbo za injili Japhet Makoye anayesomea masuala ya kilimo chuoni SUA alipozungumza na SUAMEDIA na kubainisha kuwa “ nimeamua kuimba nyimbo za injili ili nipate kufanya mahubiri kwa njia ya uimbaji nikiwa na  nia ya kuwakomboa wanadamu”.

 

Akizungumzia muziki wake kijana Makoye amesema muziki anaofanya huko katika maadhi ya zuku na rhumba na kubainisha kuwa changamoto kubwa anayokutana nayo ni kupangiwa sauti ya kuimba na prodyuza wakati akiwa ameshapanga sauti anayoona inafaa kwa wimbo husika.

Aidha msanii huyo ametoa wito kwa wasanii wote wa muziki hapa nchini kuwa na tabia ya kujifunza kupitia kwa watu wenye taaluma ya muziki ili waweze kuwa na weledi wa kutosha na muziki wanaofanya.

Kijana Makoye alinza safari yake ya muziki mwaka 2000 kipindi akiwa darasa la kwanza wakati akihudumu kwenye kwaya ya shule ya Jumapili kwenye kanisa lao mkoani Mwanza na msanii anayemvutia kijana huyo ni Mchungaji Abiudi Mishor Kutoka nchini Kongo na malengo yake ni kuwa msanii wa kimataifa.

 

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner