LATEST NEWS

Kituo cha Utafiti wa kilimo cha Mlingano kwa kushirikiana na wadau wengine wameanza utafiti wa kuwezesha zao la mkonge kuzalisha Mvinyo

Kituo cha Utafiti wa kilimo cha Mlingano kwa kushirikiana na wadau wengine wameanza utafiti wa kuwezesha zao la mkonge kuzalisha Mvinyo

18 September 2019
Kituo cha Utafiti wa kilimo cha Mlingano kwa kushirikiana na wadau wengine wa ndani na nje ya Tanzania wameanza utafiti wa kuwezesha zao la mkonge kutoa bidhaa ya Mvinyo katika zao la mkonge kutokana  na Tanzania kupata nyuzi pekee ambayo ni sa...
Readmore

Na: Alfred Lukonge

 Dar es Salaam

Mwenyekiti wa  kwaya ya uinjilisti KKKT Usharika wa Mabibo Farasi jijini Dar es Salaam Mwl. Sayuni Moses  amesema kuwa kikwazo kikubwa cha maendeleo ya kwaya nyingi ni uhaba wa kinababa walioamua kujitolea kwa dhati katika kumwimbia Mungu.

Kwaya ya uinjilisti KKKT Usharika wa Mabibo wakiwa katika moja ya huduma zao usharikani hapo.

Mwl. Sayuni amesema hayo alipozungumza na SUAMEDIA hivi karibuni na kubainisha kuwa “ changamoto  kubwa tunayokutana nayo kwenye kuiendeleza huduma hii ni upungufu wa akinababa wanaotakiwa kuimba sauti ya tatu na nne jambo linalopelekea ladha za sauti hizo kukosekana katika kwaya yetu”.

Pia Mwl. Sayuni amebainisha kuwa malengo makubwa  ya kuanzishwa kwaya  hiyo ni kutangaza injili kwa njia ya uimbaji , kurekodi sauti na video na kufanya matamasha nje ya nchi jambo ambalo anaamini litafanikiwa kwa msaada wa Mungu.

                     

                          Mwenyekiti wa kwaya ya uinjilisti KKKT Usharika wa Mabibo Mwl. Sayuni Moses.

Naye Bi. Julieth Mchomvu ambaye ni katibu msaidizi  wa kwaya hiyo amesema kuwa changamoto kubwa zinazowakumba waimbaji wengi wa muziki wa injili hapa nchini ni kukosa kujitambua wanamtumikia nani, na kutoa wito kwa waimbaji wa muziki wa injili kuwa chachu katika Kanisa na huduma kwa ujumla.

 

           Bi. Julieth Mchomvu katibu msaidizi wa kwaya ya uinjilisti KKKT Usharika wa Mabibo Farasi.                                            

Kwaya ya uinjilisti Mabibo Farasi ilianzisha tarehe 5/5/2016 ikiwa na waimbaji 10, wanawake 7 na wanaume 3 na malengo yao makubwa ni kufikisha injili sehemu isiyofikika.

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner