LATEST NEWS

Kituo cha Utafiti wa kilimo cha Mlingano kwa kushirikiana na wadau wengine wameanza utafiti wa kuwezesha zao la mkonge kuzalisha Mvinyo

Kituo cha Utafiti wa kilimo cha Mlingano kwa kushirikiana na wadau wengine wameanza utafiti wa kuwezesha zao la mkonge kuzalisha Mvinyo

18 September 2019
Kituo cha Utafiti wa kilimo cha Mlingano kwa kushirikiana na wadau wengine wa ndani na nje ya Tanzania wameanza utafiti wa kuwezesha zao la mkonge kutoa bidhaa ya Mvinyo katika zao la mkonge kutokana  na Tanzania kupata nyuzi pekee ambayo ni sa...
Readmore

Na:Adam  Ramadhan

Uongozi wa mabingwa watetezi wa Ligi ya Ufaransa, PSG umeamua kumvuta katika akademi ya klabu hiyo mshambuliaji chipukizi wa Tanzania, Haytham Saadun Hamoud mwenye umri wa miaka 17 ambaye ni mzaliwa wa jiji la Dar es Salaam.

Safari yake ya soka ilianzia katika mpango wa kuzalisha vipaji kwa klabu ya Mtibwa Sugar, baada ya hapo alielekea Oman ndipo wasaka vipaji wa PSG walipomuona.

Ameiambia Soka360 kuwa alipata fursa ya kuonekana na makocha wa PSG kwenye mashindano maalum yaliyofanyika nchini Dubai.

” Wasaka vipaji wa PSG walivutiwa na uwezo wangu kwenye mashindano maalum nchini Dubai. Mimi pamoja na wenzangu wanne kutoka mataifa mbalimbali duniani tulichaguliwa kwenda kufanya majaribio. ”

“kwa kutambua umuhimu wa fursa hii adimu, na hasa walikuwa wakitaka mtu mmoja tu, nilipambana na hatimaye kufuzu moja kwa moja kujiunga na akademi ya PSG katika kundi la chipukizi walio chini ya umri wa miaka 18. ” Anasimulia Haytham.

Haytham anaongezea kuwa wakati wa majaribio kocha wa akademi ya PSG, Andy Gill, raia wa Uingereza alivutiwa mno na uwezo wake na kumtabiria kufika mbali kama akiendelea na bidii na umakini alionao.

” Kocha Gill aliniambia haoni sababu ya mimi kutofika mbali kutokana na kile alichokiona katika miguu yangu wakati wa majaribio. ”

Licha ya kuwa na ndoto za kufanikiwa kucheza angalau moja ya ligi tano bora zaidi duniani, Haytham anasema anatamani kuja kuitumikia timu ya taifa ya Tanzania siku za usoni.

” Najiendeleza niweze kufika mbali zaidi na kuweza kuja kulitumikia taifa langu. Naomba sana Mungu anilinde na mitihani ya dunia ili nifanikishe yaliyopo moyoni mwangu.

Kwa  mujibu  wa  mtandao  wa  soka360.co.

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner