LATEST NEWS

Kituo cha Utafiti wa kilimo cha Mlingano kwa kushirikiana na wadau wengine wameanza utafiti wa kuwezesha zao la mkonge kuzalisha Mvinyo

Kituo cha Utafiti wa kilimo cha Mlingano kwa kushirikiana na wadau wengine wameanza utafiti wa kuwezesha zao la mkonge kuzalisha Mvinyo

18 September 2019
Kituo cha Utafiti wa kilimo cha Mlingano kwa kushirikiana na wadau wengine wa ndani na nje ya Tanzania wameanza utafiti wa kuwezesha zao la mkonge kutoa bidhaa ya Mvinyo katika zao la mkonge kutokana  na Tanzania kupata nyuzi pekee ambayo ni sa...
Readmore

 

SAVIO YAPANIA KUFANYA MAKUBWA MICHUONI YA KANDA TANO AFRIKA

 

Na:Alfred Lukonge

Mchezaji nguli ambaye pia ni mkufunzi wa mchezo wa mpira wa kikapu Mohamed Yusufu wa timu ya Savio amesema kuwa ana uhakika na timu yake kuchukua ubingwa wa mashindano ya kanda ya tano ya Afrika yanayotegemewa kuanza Oktoba 1 mpaka 7 katika viwanja vya ndani vya Taifa jijini Dar es Salaam.

                                                           Kikosi cha timu ya Savio kinachotegemea kushiriki mashindano ya kanda tano Afrika kuanzia Oktoba 1.

" Kwa mazoezi tunayofanya na utimamu wa kila mchezaji siku zinavyokwenda kuelekea mashindano nina imani mwaka huu mwali lazima abaki Tanzania" amebainisha Yusufu.

Pamoja na hayo Yusufu aliwataka viongozi wa mchezo huo hapa nchini kuwa na tabia ya kuutangaza mchezo huo kwani kuelekea mashindano hayo bado anaona uhamasishaji bado ni mdogo.

Timu ya Savio imepata nafasi ya kushirki mashindano hayo baada ya kuchukua ubingwa wa mashindano ya taifa ya mchezo wa mpira wa kikapu na mashindano hayo yanategemewa kushirikisha timu kutoka Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na wenyeji Tanzania.

 


 

Save

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner