LATEST NEWS

WANAFUNZI CHAGUENI KOZI KWA UMAKINI - PROF NDALICHAKO

WANAFUNZI CHAGUENI KOZI KWA UMAKINI - PROF NDALICHAKO

20 July 2019
Na Gerald Lwomile Dar es Salaam Serikali imewataka wanafunzi waliomaliza kidato cha sita nchini kuwa makini katika kuchagua kozi na kufanya udahili wa kujiunga na masomo ya juu ili kuepuka kukosa nafasi za kujiunga na vyuo hivyo kwa kukosa sifa pamoj...
Readmore
Pamoja na kutoa kozi za sayansi ya kilimo lakini pia SUA inatoa kozi mbalimbali zisizo za kilimo

Pamoja na kutoa kozi za sayansi ya kilimo lakini pia SUA inatoa kozi mbalimbali zisizo za kilimo

18 July 2019
Na Gerald Lwomile Dar es Salaam Imeelezwa kuwa pamoja na ukweli kuwa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kinatoa kozi mbalimbali za kilimo lakini pia chuo hicho kinatoa kozi katika fani mbalimbali tofauti na Kilimo kama Ualimu wa Masomo ya Sanyansi...
Readmore
Serikali inafurahishwa na hatua Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kusimamia Ithibati na Ubora wa Elimu

Serikali inafurahishwa na hatua Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kusimamia Ithibati na Ubora wa Elimu

17 July 2019
Na Gerald Lwomile Dar es Salaam Serikali imesema inafurahishwa na hatua zinazochukuliwa na Wizara ya Sayansi na Teknolojia katika kusimamia Ithibati na Ubora wa elimu unaotolewa na vyuo vikuu nchini vikiwemo vya umma na binafsi jambo linalosaidia kuw...
Readmore

Na:Adam  Ramadhan

Wafanyakazi  wa  chuo  kikuu  cha Sokoine  cha  kilimo (SUA)  wamehimizwa  kujitokeza wingi na  kushiriki   katika  michezo   iliyoandaliwa  na  idara  ya  michezo  ya  chuo  hicho  kwa   mwaka   2016, ambapo  michezo  hiyo  inatarajiwa  kuanza  Septemba  21.

Akizungumza  na  wajumbe  waliohudhuria  kikao   cha  kuandaa  mashindano  hayo  Mwenyekiti   Lwoga  Ladslaus  ambaye  pia  kiongozi   wa  Idara  ya  michezo  chuoni hapo,  amesema  kuwa  michezo  hiyo  itatoa  fursa  ya   kujenga  mahusiano  na  kufanya  afya  kuwa  bora  kwa  washiriki.

 

“Lengo  ni  kufanya  watu   wajuane  zaidi, lakini  pia  kuimarisha  afya za washiriki, hata  hivyo   idara   yetu  inakumbwa  na  changamoto  ya  fedha   ili   kuendesha mashindano  haya”, alisema Lwoga.

Aidha  wajumbe  wa  kikao  hicho   wamewataka  viongozi   wa  idara  hiyo  kuhakikisha   wanahamasisha  wafanyakazi  waweze  kuhudhuria   na kushiriki  katika  michezo  mbalimbali itakayoshindaniwa.

Michezo  hiyo  ilihairishwa  kutokana na  sababu  zilizo nje ya  uwezo  wa  idara  ya michezo  katika  chuo hicho cha  kilimo , awali michezo hiyo ilipangwa  ianze  septemba  12.

Miongoni  mwa  michezo  itakayochezwa  ni  soka, pete, mpira  wa  wavu, kuvuta  kamba,kufukuza kuku ,bao,  na  mingine.Mashindano hayo yanatarajiwa   kuanza  septemba 21 ambapo  itachukua  takribani  wiki mbili.

 

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner