NYERERE CUP KUENDELEA LEO
Na:Adam Ramadhan
Mashindano ya soka ya Nyerere Cup yaliyoanza wiki iliyopita mkoani Morogoro yataendelea tena leo kwa kuwakutanisha mafahari wawili kutoka kihonda Mlunda FC na Topsite FC katika uwanja wa sabasaba majira ya saa 10:00 alasiri.
Picha na mtandao
Hapo jana michuano hiyo iliendelea ambapo Chamwino market FC walitolewa kwa penati na timu ya Mwere FC kufuatia sare ya jumla magoli 2-2 katika dakika 90.