LATEST NEWS

Kituo cha Utafiti wa kilimo cha Mlingano kwa kushirikiana na wadau wengine wameanza utafiti wa kuwezesha zao la mkonge kuzalisha Mvinyo

Kituo cha Utafiti wa kilimo cha Mlingano kwa kushirikiana na wadau wengine wameanza utafiti wa kuwezesha zao la mkonge kuzalisha Mvinyo

18 September 2019
Kituo cha Utafiti wa kilimo cha Mlingano kwa kushirikiana na wadau wengine wa ndani na nje ya Tanzania wameanza utafiti wa kuwezesha zao la mkonge kutoa bidhaa ya Mvinyo katika zao la mkonge kutokana  na Tanzania kupata nyuzi pekee ambayo ni sa...
Readmore

Na:Ayoub Mwigune           
Ligi kuu ya Vodacom iliendelea hapo jana kwa michezo mbalimbali ambayo ilichezwa katika viwanja tofauti ambapo katika mji wa Shinyanga Stand united waliweza kuiadhibu klabu ya Azam fc kwa 1-0 na kuwafanya kushika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi wakiwa nyuma kwa alama moja nyuma ya vinara wa ligi hiyo Simba SC.


Jijini Mbeya klabu ya Mbeya City ilishindwa kutumia vyema uwanja wake wa nyumbani baada ya kukubali kichapo cha 2-0 kutoka kwa vinara wa ligi hiyo Simba sc ambapo safu ya ushambuliaji ya Simba ikiongozwa na Kichuya na Ajibu ilionekana kuwa mwiba mbele ya safu ya ulinzi ya klabu hiyo ya Mbeya city.

PICHA NA MTANDAO
Huko jijini Dar es salaam Yanga waliweza kuendeleza ushindi wake mbele ya Mtibwa sugar kutoka Turiani mkoani Morogoro ambapo waliweza kukubali kichapo cha 3-1 kutoka kwa vijana hao wenye makazi mitaa ya Jangwani.


Mbali na michezo hiyo pia kulikuwa na michezo mingine ambapo klabu ya   toka Songea ilikubali kichapo cah 1-0 kutoka kwa Kagera sugar  na kuwafanya waendelee kushika nafasi ya mwisho katika msimamo wa ligi ,Mwadui aliweza kuondoka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Africa lyon ,wakati Ruvu stars wakitoka sare ya bila kufungana dhidi ya maafande Tanzania Prison.


Kwa matokeo hayo klabu ya simba bado inaongoza katika msimamo wa ligi kwa kuwa na alama 20 ikifutiwa na klabu ya Stand united  ikiwa na alama 19 wakati klabu ya majimaji inashikilia mkia ikiwa na alama tatu ikifuatiwa na klabu ya toto Africa ambayo ina alama nane.

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner