LATEST NEWS

NDAKI YA TIBA ZA MIFUGO NA SAYANSI ZA AFYA IMETAKIWA KUTUMIA VYOMBO VYA HABARI ILI WANANCHI WAWEZE KUFAHAMU SHUGHULI WANAZOFANYA- DR HENRY BWILLE

NDAKI YA TIBA ZA MIFUGO NA SAYANSI ZA AFYA IMETAKIWA KUTUMIA VYOMBO VYA HABARI ILI WANANCHI WAWEZE KUFAHAMU SHUGHULI WANAZOFANYA- DR HENRY BWILLE

01 November 2019
Na Amina Hezron,Morogoro Mwenyekiti wa Ndaki ya Tiba za Mifugo na Sayansi za Wanyama VET ameitaka ndaki hiyo kujitangaza kupitia vyombo vya habari ili wananchi waweze kufahamu shughuli zinazofanywa na ndaki hiyo na jamii kuweza kufaidika. Akizungumza...
Readmore
WAZIRI WA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA PROF. JOYCE NDALICHAKO AMEZITAKA TAASISI ZA ELIMU NCHINI KUWA MSTARI WA MBELE KATIKA KUIMARISHA SEKTA YA MICHEZO

WAZIRI WA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA PROF. JOYCE NDALICHAKO AMEZITAKA TAASISI ZA ELIMU NCHINI KUWA MSTARI WA MBELE KATIKA KUIMARISHA SEKTA YA MICHEZO

01 November 2019
Na AYOUB MWIGUNE NA AMINA HEZRON Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amezitaka Taasisi za Elimu nchini kuwa mstari wa mbele katika kuimalisha sekta ya michezo kwenye Taasisi  kwani kutaimalisha afya pamoja na kuinua viwa...
Readmore
SHULE ZOTE ZENYE MCHEPUO WA KILIMO NCHINI KUHAKIKISHA ZINAKUWA NA UWEZO WA KUZALISHA MAZAO YA CHAKULA- PROF. NDALICHAKO

SHULE ZOTE ZENYE MCHEPUO WA KILIMO NCHINI KUHAKIKISHA ZINAKUWA NA UWEZO WA KUZALISHA MAZAO YA CHAKULA- PROF. NDALICHAKO

01 November 2019
Na: Gerald Lwomile Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesema itahakikisha shule zote zenye mchepuo wa Kilimo nchini kuhakikisha zinakuwa na uwezo wa kuzalisha mazao ya chakula kwani hiyo ndiyo njia sahihi ya kufahamu kilimo na n...
Readmore
VIDEO:Multisectoral research on sleeping sickness in Tanzania in the context of climate change

VIDEO:Multisectoral research on sleeping sickness in Tanzania in the context of climate change

01 November 2019
Professor Paul Gwakisa of Sokoine University of Agriculture in Tanzania engaged a “OneHealth” approach to research on sleeping sickness, bringing together the health, environment and agriculture sectors. Professor Gwakisa has conducted his research w...
Readmore

Na: Kizito Natharine Ugulumo

 

ARDHI ni rasilimali muhimu kwa maendeleo ya jamii katika kujiletea maendeleo kwa kuitumia  kuendeshea shughuli za maendeleo ikiwemo kilimo,ujenzi wa makazi,ufugaji na shughuli zingine hivyo kutokana na umuhimu wake baadhi ya viongozi  kwenye vitongoji na vijiji wamekuwa wakitumia  umuhimu wa mahitaji ya ardhi kwa jamii kujinufaisha kwa kugawa ardhi bila kuzingatia sheria ,sera na kanuni zilizopo za ugawaji ardhi.

 

Hali hiyo imekuwa ikipelekea kuibuka kwa migogoro ya ardhi  mara kwa mara katika maeneo mbalimbali nchini na kwamba miongoni mwa sababu zinazochangia migogoro hiyo ni baadhi ya viongozi wa vijiji na vitongoji  kutaka kuingia madarakani kwa kutaka kujinufaisha ni miongoni mwa sababu zinazochangia kishamili kwa migogoro ya ardhi nchini.

 

Katika miaka ya 1990 serikali ya Tanzania ilijihusisha katika mchakato wa kutengeneza sera na mfumo wa kisheria ambayo ilipelekea  uundaji wa sera ya Taifa ya ardhi ya mwaka 1995 na kutungwa kwa sheria ya ardhi ya mwaka 1999 ambazo ni Sheria ya ardhi ya vijiji namba tano ya mwaka 1999 na sheria ya ardhi namba nne ya  mwaka 1999 zimekuwa zikieleza mpango wa matumizi bora ya ardhi kwenye vijiji lakini licha ya kuwepo kwa sheria hizo bado changamoto ya migogoro ya ardhi imeendelea kujitokeza.

 

 Hata hivyo juhudi hizo  bado zinahitajika katika kukuza uelewa wa wanakijiji juu ya mifumo ya kisheria katika masuala ya haki za ardhi,uwezo wa uwekezaji mkubwa wa kilimo na uhusiano na ustawi wa wakulima wadogo,kilimo endelevu na maendeleo endelevu ya nchi kwa ujumla.

 

Migogoro hiyo ya ardhi mingi imekuwa ikitokeza baina ya wakulima na wafugaji,wakulima na wawekezaji, mtu kwa mtu na kijiji kwa kijiji ambayo wakati mwingine imekuwa ikipelekea watu kupoteza maisha ,kupata ulemavu na upotevu wa  mali zao.

 

Kushamili kwa migogoro hiyo imekuwa ikisababisha kudumaa kwa uchumi kwa wananchi kwani wakati mwingine wakulima wamekuwa wakishindwa kuzalisha mazao,wafugaji mifugo yao kujeruhiwa,wawekezaji nao mali zao kuharibiwa na wananchi kutokana na kugombea ardhi kwa ajili ya kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwemo kilimo,mkazi na ufugaji.

 

Akizungumza na Mwandishi wa Makala haya mratibu wa Mtandao wa Mashirika  yasiyokuwa ya Kiserikali yanayofanya kazi na wakulima na wafugaji wadogo nchini Tanzania(PELUM Tanzania) bw Donati Senzia  kwa upande wao wanaiona changamoto  hiyo kuwa ni kikwazo kwa wakulima na wafugaji wadogo katika kuendeleza shughuli zao na kuona haja ya  kuanzisha mradi wa Ushiriki wa wananchi katika  Usimamizi wa shughuli za serikali (Citizen Engaging In Government Oversight-CEGO)  katika sekta ya Kilimo kwa ufadhili wa shirika la Maendeleo la Misaada la Watu wa Marekani Tanzania(USAID) unaotekelezwa kwa miaka minne kuanzia Desemba 2013hadi Desemba 2017.

 

Senzia anasema PELUM Tanzania inatekeleza mradi wa CEGO katika kilimo kwa kushirikiana na mashirika wanachama matatu ambayo ni UMADEP Morogoro na TAGRODE Iringa na INADES Formation Tanzania Dodoma.

 

Anasema mradi huo unatekelezwa katika ijiji 30 kwenye mikoa  Mitatu yaani Dodoma,Iringa na Morogoro katika halmashauri za wilaya za Mvomero  na Morogoro mkoani Morogoro,wilaya za Bahi na Kongwa mkoani Dodoma na wilaya za Kilolo na Mufindi mkoani Iringa.

 

Kwa upande wa halmashauri ya wilaya ya Morogoro  mradi unatekelezwa katika vijiji vya Lubungo,Mikese mjini,Newland,Luholole na Mfumbwe.

 

Anasema  kupitia mradi wa CEGO wananchi wameweza kupata mafunzo ambapo   watu 2,744 wamenufaika na mafunzo hayo  kati ya hao watu 1630 ni wanaume sawa na asilimia 59.5 na wanawake 1,114 sawa na asilimia 40.5 .

 

Mradi huo katika mikoa ya Dodoma  unatekelezwakwenye wilaya za Kongwa na Bahi,Iringa katika wilaya za Mufindi na Kilolo) na Morogorokatika wilaya za Morogoro na Mvomero katika vijiji 30.

 

Anasema katika mkoa wa Morogoro jumla ya watu 901 kati yao wanaume 517 na wanawake 384 wamepatiwa mafunzo ya haki za ardhi na utawala vijijini na ambapo  kwa  halmashauri ya Morogoro wananchi wapatao471 kati yao wanaume 271 na wanawake 192 wamefikiwa na mafunzo hayo.

 

Miongoni mwa watu hao waliopatiwa mafunzo hayo ni pamoja na watumishi wa serikali wakiwemo watendaji kata,watendaji wa vijiji,maafisa ugani,fundi sanifu ramani) ambao ni watu 12 wakiwemo wanaume 8 na wanawake 4,Mabaraza ya ardhi ya vijiji na kata watu 58 kati yao wanaume 25 na wanawake 33,halmashauri za vijiji 5 wajumbe 139 wakiwemo wanaume 94 na wanawake 19 na wananchi wa kawaida watu 218 wakiwemo wanaume 127 na wanawake 91.

 

Mafunzo hayo yalihusisha Haki za Ardhi kwa makundi mbalimbali,sera na sheria zinazosimamia ardhi,Mpango wa Matumizi ya ardhi vijijini,Utatuzi wa Migogoro ya ardhi naya utawala na Usimamizi wa Rasilimali Tanzania  ambayo yalilenga  hasa kuwajengea uelewa wananchi katika masuala ya haki za ardhi na kuwajengea uwezo zaidi katika kuisimamia serikali katika usimamizi wa ardhi na rasilimali za nchi.

 

Pamoja na mafunzo hayo jumla ya machapisho ya aina tatu yalitolewa ambapo nakala 12,000 zilichapishwa na kusambazwa  kwa wananchi ambazo zinahusu haki ya kupata na kutumia ardhi,Haki za ardhi kwa wanawake na utatuzi wa Migogoro ya ardhi Tanzania  ambapo kwa upande wa halmashauri ya wilaya ya Morogoro vitabu  zaidi ya 1200 vilisambazwa kwa wananchi.

 

PELUM Tanzania ulianzishwa mwaka 1995 na kusajiliwa kama mfuko wa udhamini mwaka 2002,mwaka 2008 PELUM Tanzania ilisajiliwa  chini ya wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na watoto na kwamba Mashirika wanachama wa PELUM Tanzania kwa sasa ni 37 ambayo yanahudumia wakulima na wafugaji wadogo katika mikoa yote ya Tanzania Bara.

 

Sudi Mpili na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya morogoro anasema wananchi wengi ni wakulima na wafugaji na kwamba shughuli zao kubwa zinahitaji ardhi kwa ajili ya kuendesha shughuli hizo hivyo mara nyingi wamekuwa wakiingia kwenye migogoro kutokana na kuwepo mwingiliano baina ya pande hizo mbili.

 

Hali hiyo imekuwa ikichangia wakati mwingine wakulima na wafugaji  kuingia katika mapigano baina ya pande hizo mbili na kusababisha baadhi ya wananchi kupoteza maisha na mali zao huku wengine wakibakia na ulemavu wa kudumu.

 

Bi Regina Chonjo ni mkuu wa wilaya ya Morogoro anasema zaidi yaasilimia  78 ni wakulima hivyo bila kusaidia kutatua changamoto za migogoro ya ardhi wananchi hao wataweza kujipatia kipato kupitia sekta ya kilimo na kutekeleza mpango wa kuufanya mkoa wa Morogoro kuwa ghala la Chakula.

 

Anasema viongozi wa vijiji wanaopata elimu hiyo watumia nafasi yao katika kutatua changamoto ya migogoro ya ardhi kwenye maeneo yao na sio kuwa chanzo cha kushamili kwa migogoro ya ardhi kwenye maeneo yao.

 

Anasema katika wilaya ya Morogoro kumekuwa na migogoro ya ardhi na kwamba tarafa za Bwakira na Mvuha zimekuwa zikiongoza katika kukithiri kwa migogoro ya ardhi na kwamba hali hiyo imekuwa ikisababisha wakulima na wafugaji kuishi katika uhasama mkubwa.

 

Viongozi watumia nafasi walizonazo kwenye vijiji vyao katika kusaidia kutatua changamoto ya migogoro ya ardhi ili kuwezesha wananchi kuweza kuishi kwa amani na utulivu kwa ajili ya manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo vya taifa.

 

Anasema kuna haja kwa PELUM Tanzania kuna haja kuangalia uwezekano wa kuendelea kutoa elimu katika maeneo mingine ya wilaya hiyo kutokana na kukithiri kwa migogoro ya ardhi katika baadhi ya maeneo na hivyo kuwa kikwazo katika kukuza uchumi wa wananchi.

 

“kwa sasa kuna uhasama mkubwa hali ambayo inawafanya wananchi kutokuwa tayari kushirikiana na upande mmoja kwani wafugaji na wakulima kwa sasa si ndugu tena wa kuishi pamoja kwani mkulima akimuona mfugaji anasema huyo kafuata nini hapa na mfugaji akimuona mkulima anasema mkulima amefuata nini hapa”anasema Chonjo.

 

 Anawaomba PELUM Tanzania kushuka chini katika Programu zao kwa kuzungumza na wananchi vijijini ambako kunaonekana kuna matatizo ili kuweza kuwafikia moja kwa moja wananchi na  kuwasaidia wananchi kwani kila Mwananchi anamtegemea mwenzake katika kuishi kwa kuishi kwa amani.

 

  Bw Ramadhani Simba katibu baraza la ardhi kata ya Mikese anasema migogoro mingine inachangiwa na viongozi wa vijiji kugawa ardhi mara mbili lakini fedha pia wanakuwa nazo viongozi licha ya kwamba sheria zinaeekeza wazi kuwa asilimia kumi na fedha za kuuzwa ardhi zinabaki kwenye kijiji husika.

 

Halima Bakari mabaraza ya ardhi ya kata viongozi wa vijiji kuuza ardhi mara mbili kwa watu tofauti,wengine kutengeneza hati bandia ili kuweza kujipa uhalali wa kumiliki ardhi hata kama ardhi hiyo si yake kisheria.

 

Anasema pia tatizo la wanaume kuwadharau wanawake kumiliki ardhi kwenye ardhi za ukoo kwa kuwaona kuwa wanawake hawana haki ya kumiliki ardhi kisheria licha ya sheria kueleza wazi kuwa mwanamke naye ana haki ya kumiliki ardhi sawa na mwanaume.

 

Anaomba elimu zaidi kutolewa na PELUM,wadau wengine na serikali ili kuondoa mtizamo uliopo katika jamii kulingana na mila na desturi kwa kuona kuwa mwanamke hana haki ya kumiliki mali hususan ardhi sawa kama ilivyo kwa wanaume.

 

Abdu Chimali  mkazi wa Mfumbwe wilayani Morogoro  ni Mwananchi anasema baadhi ya viongozi kutojua majukumu yao kama viongozi katika kuongoza wananchi hali hiyo  inachangia viongozi hao kutotambua wajibu wao na mipaka yao ya kiutendaji.

 

Anasema hali hiyo imekuwa ikisababisha baadhi ya viongozi wa vitongoji na vijiji kugawa ardhi bila kuzingatia sheria kuwa maamuzi ya kutoa ardhi ya kijiji hutolewa kwenye mkutano mkuu wa kijiji baada ya muombaji kuandika barua ya kuomba ardhi  na wananchi  baada ya kukubali hutoa ruhusa ya kutoa ardhi kwa muombaji.

 

Lakini hata hivyo ardhi inayotolewa na kijiji haizidi ekari 50 na kwamba zaidi ya kiwango hicho muombaji anapaswa kwenda ngazi ya halmashauri lakini baadhi ya viongozi kwenye vitongoji au vijiji kutokana na baadhi yao kutokuwa na uelewa huo au kufanya hivyo kwa tamaa hutoa ardhi zaidi ya ekari 50 kwa muombaji.

 

Mchungaji Steven Simkoko anasema tatizo la rushwa miongoni mwa viongozi wa vitongoji na vijiji kumekuwa kukichangia kukithiri kwa migogoro ya ardhi kwenye baadhi ya maeneo nchini.

 

Anasema Pia sheria za ardhi pamoja na sera hazieleweki kwa wananchi na viongozi jambo ambalo limekuwa likichangia viongozi na wananchi kushindwa kuzitekeleza sheria hizo na kupelekea kushamili kwa migogoro ya ardhi kwenye vijiji.

 

Omari Mbega ni Mwenyekiti wa Baraza la ardhi la wilaya ya morogoro anasema kuna migogoro mingine inajitokeza kwa baadhi ya watu kung’ang’ania ardhi ambayo si yake kisheria licha ya kwamba wanafahami hilo.

 

“hivi kwa nini mtu ung’ang’anie ardhi ambayo si yake lengo likiwa ni kutaka kuendelea kuwepo kwenye eneo ambalo umekuwa ukiishi hapo wakati mtu una uwezo wa kwenda eneo lingine nje ya ulipozaliwa na kuendesha maisha kama kawaida kuliko kung’ang’ania ardhi ambayo unafahamu fika si yako”anasema Mbega.

 

Anasema migogoro mingine  ya ardhi inachangiwa na baadhi ya wenye maeneo makubwa ambayo wanayamiliki kisheria kutoyaendeleza hali ambayo inasababisha baadhi ya wananchi wanaokosa ardhi kuyavamia maeneo hayo.

 

Pia wakati mwingine baadhi ya taasisi,mashirika na makampuni yanapofanya shughuli za maendeleo kutumia ardhi bila kuwalipa  wananchi fidia ya ardhi yao waliyoichukua licha ya wananchi hao kufanya maendeleo kwenye ardhi hiyo.

 

Wanasiasa nao wameelezwa wakati mwingine kuingia migogoro ya ardhi kwa kutoa maamuzi bila kuzingatia sheria hali ambayo imekuwa ikichangia wananchi kuingia kwenye migogoro baina ya wao kwa wao,wananchi na wawekezaji au kijiji na kijiji.

 

Anasema tatizo lingine ni baadhi ya jamii kuwanyanyasa ndugu zao hasa wanawake kwa kuwanyima mali za urithi kwa kuona kuwa wanawake hawana haki ya kumiliki mali hasa ardhi.

 

Greson Angolile  afisa Programu PELUM Tanzania anasema  mwaka 2014 Mtandao wa PELUM ulifanya   utafiti  na kuibaini changamoto za migogoro ya ardhi  baina ya wakulima kwa wakulima ,wakulima na wafugaji, vijiji na vijiji katika masuala ya mipaka kwani baadhi ya vijiji vinaanzishwa bila kuinisha mipaka.

 

Angolile anasema Chanzo kingine  cha migogoro ni ongezeko la mifugo,kuongezeka kwa soko la ardhi hali ambayo inasababisha baadhi ya watu kutoka maeneo mbalimbali kuja kununua ardhi vijijini lakini pia baadhi ya ardhi kuhodhiwa na wachache bila kuendelezwa na kupelekea wananchi kuvamia ardhi hizo.

 

Anasema tatizo kubwa ni  eneo kubwa la ardhi  ya Tanzania kwenye vijiji kutopimwa hali ambayo inachangia migogoro ya ardhi kwani kufanya hivyo kutasaidia kuainisha mpango wa matumizi bora ya ardhi kwenye kila vijiji.

 

Pia kuna tatizo wananchi kutokuwa na elimu katika suala zima la matumizi bora ya ardhi  hivyo jitihada zaidi zinahitajika katika kutoa elimu kwa viongozi kwenye vijiji,vitongoji na jamii kwa ujumla.

 

Kuwepo na mawasiliano katika sekta za serikali katika kupanga mipango ya matumizi bora ya ardhi ili kuweza kushirikiana katika utekelezaji wa shughuli za kupanga mipango ya matumizi bora ya ardhi.

 

 

 

 

 

 

 

 

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner