LATEST NEWS

Kituo cha Utafiti wa kilimo cha Mlingano kwa kushirikiana na wadau wengine wameanza utafiti wa kuwezesha zao la mkonge kuzalisha Mvinyo

Kituo cha Utafiti wa kilimo cha Mlingano kwa kushirikiana na wadau wengine wameanza utafiti wa kuwezesha zao la mkonge kuzalisha Mvinyo

18 September 2019
Kituo cha Utafiti wa kilimo cha Mlingano kwa kushirikiana na wadau wengine wa ndani na nje ya Tanzania wameanza utafiti wa kuwezesha zao la mkonge kutoa bidhaa ya Mvinyo katika zao la mkonge kutokana  na Tanzania kupata nyuzi pekee ambayo ni sa...
Readmore

Na:Adam Ramadhan

Muimbaji  na  mtayarishaji  wa  muziki  wa Bongo fleva  nchini Tanzania Elias Barnabas  alimaarufu  kama Barnaba Classic  amesema  kuwa  albamu  yake  mpya itatoka kabla  ya mwezi  wa  tano  huku  akiorodhesha baadhi ya wasanii watakaokuwepo  katika nyimbo  zinazopatikana katika albamu hiyo.

Akizungumza  kwa  njia ya  simu katika kipindi  cha njendani kinachorushwa  na  Suafm, muimbaji  huyo  amesema albamu  yake itaitwa nanenane huku akiwa ameshirikisha wasanii kadhaa kama Maua Sama, Juma Musa alimaarufu kama Jux, Sunday  Mjeda alimaarufu  kama Linex  na wengineo.

 

                                                                                                                                      Picha na mtandao.

Hata hivyo  aliongeza  siku  za  hivi  karibuni  ataachia  wimbo  wake  mpya  ambao utakwenda  kwa  jina la Lonely  ikiwa  ni audio na video.

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner