Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA wachangia damu lita 25

Josephine Mallango

Morogoro

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA wamechangia lita 25 za damu ambazo zitaweza kuokoa maisha ya watoto wenye umri chini ya  miaka 5 wasiopugua 50.

Zoezi hilo la uchangiaji wa damu limefanyika SUA lililoandaliwa na  Serikali  ya Wanafunzi SUA “SUASO” pamoja na Klabu ya  inayojishughulisha na kuhamasisha watu kuepuka Ukimwi “SUA  AIDS CLUB” likiwa na lengo la wanafunzi kutambua afya zao mapema sambamba na uchangiaji wa damu kwa ajili ya watu wenye uhitaji.

uchangiaji damu wanafunzi

Wanafunzi mbalimbali wa SUA wakiwa tayari kuchangia damu ( Picha na Josephine Mallango)

Akizungumza na SUAMEDIA  Waziri wa Afya wa serikali ya wanafunzi SUA Bw. Charles Makongo amesema wamekuwa wakiandaa mabonanza  kama sehemu ya ushawishi kusaidia wanafunzi kutambua afya zao kwa kupima VVU na kuchangia damu kwani michezo imekuwa ikipendwa na kukusanya watu kwa urahisi.

``… upimaji wa afya wa mapema  una faida kwa maisha ya kila siku  ya mtu yoyote tukiwemo wanafunzi  kwa kuwa unampa  mtu nafasi ya kujua hali yake na namna ya kukabiliana nayo,….. na ikumbuke kuzuia ni rahisi kuliko kutibu, wakati wingine  vilevile kutambua tatizo mapema kuna nafasi kubwa ya kupata ufumbuzi wa mapema ukiwa unaendelea na maisha mengine``     

Waziri huyo wa afya wa Serikali ya Wanafunzi akiendelea kufafanunua kuhusu lita hizo 25 za damu amesema pamoja na kuokoa watoto wapatao 50, pia inaweza kuokoa watu wazima wasiopungua 25, wajawazito 25, ikimaanisha watu 50.

Kwa upande wake mwenyekiti wa klabu ya “SUA AIDS” Bw. Boniphace Vitus amesema bonanza hilo limekuwa na mafanikio tofauti na lile la tarehe 1/12/2018 ambayo ni siku ya ukimwi duniani kwa kuwa walipata damu lita 12 tu huku bonanza hili wakipata damu lita 25

uchangiaji damu wanafunzi watoa huduma

Baadhi ya wanafunzi wa SUA wakiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa masuala ya damu ambao walikuja kusaidia zoezi la uchangiaji wa damu (Picha na Josephine Mallango)

Amesema katika upimaji wa VVU walijitokeza  zaidi ya watu 45  na kwamba  wanatarajia kufanya bonana jingine mwezi wa 4  siku ya Sokoine, huku akiwahimiza wanafunzi kujitokeza kwa wingi sambamba na wanajumuhiya wa SUA.

SCALE-N yanufaisha wananchi wa hali ya kawaida mkoani Dodoma

Gerald Lwomile

Dodoma

Kikundi cha wawezeshaji wananchi kilichopata mafunzo kutoka mradi wa SCALE-N uliotekelezwa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA katika kijiji cha Chinoje wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma kimesema kuwa mradi huo kwa kiasi kikubwa utainua maisha ya wananchi ambao wanapata mafunzo ya kilimo mseto/anuai

Hayo yamesemwa na wawezeshaji Bibi Lucy Mgalonje ambaye pia ni katibu wa kikundi cha wawezeshaji hao na Bw.Yona Matogwa wakati wakiongea na SUAMEDIA katika kijiji cha Chiloje.

IMG 9258

Moja ya mbogamboga ikiwa imestawi vizuri juu ya kiroba katika kijiji cha Chinoje ( Picha na Gerald Lwomile)

Wamesema kupitia mradi huo wamejifunza mambo mengi ambayo yatawanufaisha wananchi na hasa masuala ya lishe na kilimo cha bustani mbogamboga na matunda.

Bibi Mgalonje amesema kuwa hivi sasa wanapita katika kaya mbalimbali na kutoa elimu ya lishe, ulimaji wa bustani za mboga nyumbani na shuleni, namna ya kukausha mazao ya mbogamboga na kilimo matunda.

IMG 9244

Tunda aina la Tikiti lililolimwa na wakulima likiwa limestawi katika kijiji cha Chinoje Mkoani Dodoma (Picha na Gerald Lwomile)

 “Tuna jukumu kubwa la kwenda katika kila kaya, kuhakikisha kila kaya inapata elimu ya lishe na inawafikia kwa kiwango kama tulichofundishwa kila mtu apate elimu ya lishe” amesema Bibi Mgalonje

Naye Bw. Yona Matogwa ambaye pia ni mjumbe katika mradi kikundi hicho amesema kuwa elimu wanayotoa imekuwa ikipokelewa na watu mbalimbali wakiwemo wanaume ambao sasa wameamka

“ Nasema hivi kwa kuwa mimi ni mwanaume na nimeupokea mradi huu… na ukiangalia katika kila kaya ninayofundisha baba ndiyo anakuwa wa kwanza na hii inamsababisha mama haendi mbali kuchuma mboga” amesema Bw. Matogwa

Akizungumza na SUAMEDIA Dk. Hadijah Mbwana mtafiti katika mradi huo kutoka SUA amesema kuwa SUA kupitia mradi huo imewawezesha wananchi wa kijiji cha Chinoje mkoani Dodoma na hasa kina mama kuwa na uhakika wa upatikanaji wa maji safi na salama ambapo awali walikuwa wakifuata maji hayo umbali mrefu.

HADIJA PICHA

Dr. Hadijah Mbwana wa SUA aliyejifunga ushungi akitoa maelezo juu ya mradi wa SCALE-N ulivyopokewa na wananchi wa Chiloje katika siku ya ufunguzi wa jengo na kisima cha maji, kushoto aliyevaa kofia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Chakula na Kilimo wa Ujerumani Bw. Michael Stubgen ( Picha na Gerald Lwomile)

Mradi wa SCALE-N ambao ulitekeleza fursa za lishe muhimu na kilimo mseto/anuai ili kuongeza uhakika wa chakula yaani SCALE-N uliotekelezwa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA na nchi ya Ujerumani.

SUA kupitia ICE kuendelea kushirikiana na wahitimu wajasiliamali

Ayoub Mwigune

Morogoro

Imeelezwa kuwa elimu inayotolewa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA imewajengea uwezo wanafunzi wanaohitimu katika chuo hicho kuweza kujiajiri wenyewe na kufanya chuo hicho kuwa tofauti na vyuo vingine.

Hayo yameelezwa na Dk. Innocent Babili ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Ugani kilichopo chini ya Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza ICE iliyopo SUA wakati akizungumza na SUAMEDIA ofisini kwake.

ICE

Dk. Babili amesema kuwa kupitia mafunzo yanayotolewa SUA wahitimu mbalimbali wamefanikiwa kufungua makampuni makubwa na kutolea mfano wa kampuni ya  Shambani Milk ambayo yamechangia ongezeko la ajira nchini.

“Elimu inayotolewa na SUA imewajengea uwezo wahitimu wa kujiajiri wenyewe kwa mfano kampuni ya Shambani Milk ambayo wanasindika maziwa” Amesema Dk. Babili.

Pia Dk. Babili amesema kuwa SUA imekuwa na ushirikiano mzuri na wanafunzi ambao wamehitimu chuoni hapo na kujiajiri wenyewe kwa kuweza kuwatumia katika maonesho mbalimbali ambayo chuo kimekuwa kikishiriki yakiwepo maonesho ya wakulima na maonesho ya kumbukizi ya Sokoine ambayo hufanyika kila mwaka chuoni hapo.

Katika hatua nyingine  Dk. Babili  amesema kuwa chuo kimeendelea kupokea wageni  wengi  kutoka  mashirika, kampuni  na  vyuo mbalimbali ambao wamekuwa wakifika chuoni hapo kwa lengo la kujionea na kujifunza kuhusu kilimo  pamoja na kuhudhuria katika kozi fupi ambazo zimekuwa zikitolewa.

Jamii yatakiwa kubadili mtazamo hasi kuwa wanawake sio muhimu

Josephine Mallango.

Kilombero

Jamii  imeshauriwa  kubadili  mtazamo hasi  dhidi ya wanawake kuwa wao sio muhimu katika kuleta maendeleo na kwamba wanawake hawana  mchango katika kuchangia shughuli za  kimaendeleo  na badala yake   inapaswa kuwathamini na kuwashirikisha  katika kuibua, kuandaa mpango, kutekeleza, kufuatilia na kupata mrejesho wa mpango wa shughuli za maendeleo kuanzia ngazi ya familia, kitongoji, kijiji/mtaa, kata, wilaya, mkoa na taifa kwa ujumla   kutokana na ukweli kwamba wanawake wana uwezo sawa na wanaumwe katika kufanya shuguli za kimaendeleo .

maandamano raawu

Wanawake wakiwa katika maandamano ya siku ya wanawake duniani wilayani Kilombero. (Picha na Calvin Gwabara)

Viongozi wamewataka wanawake kuachana na fikra za kimazoea za kuendelelea  kubagua kazi za kufanya kwa kuwa katika karne hii ya sayansi na teknolojia kazi zote zinaweza kufanywa na kila mmoja bila kujali ni mwanamke au mwanaume.

Wakizungumza katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Viongozi wa ngazi mbalimbali mkoani Morogoro akiwemo Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dr. Kebwe Steven Kebwe ambaye aliwakilishwa na Mkuu wa wilaya ya Ulanga Mh. Ngollo Malenya kwenye maadhimisho ya hayo amesema jamii inapaswa kubadili mtazamo hasi ulipoo dhidi ya wanawake kuwa hawana mchango katika kuleta maendeleo.

“Katika kuelekea Tanzania ya viwanda  dhana halisi inaanza kuonekana kwani  wanawake wanaendelea na kasi kubwa ya kujituma na kuthubutu na sasa wanawake wengi   wanamiliki viwanda vikubwa , vya kati na vidogo na kuna uwezekano mkubwa wa wanawake kuja  kutoa ajira nchini .” Amesema Mh. Ngollo Malenya

Mkuu wa wilaya ya malinyi Mh.Majura Kusika amesema kabla ya kuanza kwa sherehe za maadhimisho hayo waliweza kutembelea mabanda mbalimbali ambapo wamejionea bidhaa mbalimbalia zikiwa katika ubora  na vifungashio vinavyoendana na tekinolojia iliyopo jambo linaloonesha  wazi  Tanzania ya viwanda inatekelezwa kwa kiasi kikubwa na wanawake.

 

Wanawake RAAWU

Wanawake wa RAAWU mkoa wa Morogoro  wakifuatilia wakisikiliza hotuba mbalimbali katika sherehe ya siku ya wanawake duniani.  (Picha na Calvin Gwabara) 

 

Amesema wakati wanawake wakiadhimisha siku hii hainabudi kuishukuru serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli   na makamu wake  Mh. Samia Hassan Suluhu ambaye ni mwanamake  na kama nchi wanajivunia kuwa na  mwanamke kwenye  nafasi ya juu katika uongozi wa Taifa  na kwamba serikali  inaendelea kutekeleza mikataba mbalimbali ya kimataifa, kitaifa na kikanda pamoja na sera mbalimbali zinazolenga kuwainua wanawake ili kulinda na kutetea haki za wanawake zinazokandamizwa na jamii kupitia sheria mbalimbali .

Kwa upande wake  Mlezi kamati ya wanawake RAAWU kutoka SUA  Prof. Yasinta Muzanila amesema kupitia kauli mbiu ya mwaka huu ya “BADILI FIKRA KUFIKIA USAWA WA KIJINSIA KWA MAENDELEO ENDELEVU” ni wakati wa wanawake sasa kubadilika  kifikra kwa kuachana na fikra za kimazoea za kubagua kazi na badala yake amewasisitiza washiriki kikamilifu ili kufikia maendeleo, lakini pia akisema usawa wa kijinsi hauwezi kufikiwa endapo hakutakuwa na juhudi za makusudi katika kumwinua mwanamke.

mlezi wanwake RAAWU. SUA

Mlezi wa wanawake RAAWU SUA  Prof. Yasinta Mzanila akizungumza na wanawake wa RAAWU mkoa wa Morogoro  (Picha na Calvin Gwabara)

Nae  kaimu katibu wa RAAWU Mkoa wa morogoro ambaye pia ni  mwenyekiti wa tawi la RAAWU sua Bi. Gaudensia Donati amewakumbusha wanawake wote wakati  wakidai usawa  chachu iwe  usawa  wa pande mbili  hivyo wasijisahau na kuwanyanyasa wenza wao kwa  kuangalia usawa  katika upande mmoja pekee.

mwenyekiti wa RAAW . SUA

Kaimu Katibu wa RAAWU mkoa Bi. Gaudensia Donati akizungumza katika hafla ya siku ya wanawake duniani wilayani Kilombero (Picha na Calvin Gwabara)

Kila mwaka ifikapo tarehe 8 ya mwezi Machi wanawake kote ulimwenguni huungana  kusherekea siku hiyo ya wanawake duniani ambapo nchini Tanzania sherehe hizo kitaifa hufanyika kila baada ya miaka mitano lakini kukiwa na fursa kwa kila mkoa kusherehekea siku hiyo katika  ngazi ya mkoa na wilaya kwa kila mwaka. Mkoani Morogoro kwa mwaka 2019 sherehe hizo katika ngazi ya mkoa  zilifanyika wilayani Kilombero.

Watanzania wametakiwa kuhakikisha wanalichukulia suala la lishe kama jambo la msingi

Na Gerald Lwomile

Dodoma

Watanzania wametakiwa kuhakikisha wanalichukulia suala la lishe kama jambo la msingi ili kuhakikisha wanakuwa na afya bora na itakayowafanya kufanya kazi kwa manufaa ya nchi yao.

Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni mkoani Dodoma na Katibu Mkuu wa Wizara ya Chakula na Kilimo wa Ujerumani Bw. Michael Stubgen wakati akikagua mradi wa kutekeleza fursa za lishe muhimu na kilimo mseto/anuai ili kuongeza uhakika wa chakula yaani SCALE-N uliotekelezwa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA na nchi ya Ujerumani.

katibu mkuu akikata utepe
Katibu Mkuu wa Wizara ya Chakula na Kilimo wa Ujerumani  Bw. Michael Stubgen akikata utepe kuashiria kuzindua kisimacha maji katika  kijiji cha Chinoje  , kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Prof. Siza Tumbo. (Picha na Gerald Lwomile)
 

Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Chakula na Kilimo wa Ujerumani amesema hivi sasa tatizo la lishe ni kubwa duniani na hata nchi yake ya Ujerumani inakumbwa na tatizo hilo ambapo watu wengi hawajui lishe bora.

Hivi sasa tatizo la lishe ni kubwa sana na huwezi amini kuwa hivi sasa hata nchini Ujerumani kumekuwa na tatizo kubwa la watu kushindwa kula mlo kamili na kweli niwapongeze kwa kutafuta njia rahisi za kutatua tatizo hili kwa watanzania amesema Michael Stubgen.

Awali akizungumzia mradi huo mkuu wa mradi Dk. Khamaldin Mutabazi amesema katika kutekeleza mradi huo wakulima hodari wanane walichaguliwa na kufundishwa njia na mbinu za kuwafundisha wakulima wengine kuu ya elimu ya lishe, ulimaji wa bustani za mboga nyumbani na mashuleni, namna ya kukausha mazao ya mbogamboga na kilimo matunda.

Amesema kuwa pamoja na kufundishwa mbinu hizo wakulima hao wamewezeshwa kwa kujengewe kituo cha lishe na biashara kwa ajili ya mafunzo na ofisi ambapo wananchi wengi zaidi wameendelea kunufaika na mradi huo.

katibu mkuu akipata maelezo

Katibu Mkuu wa Wizara ya Chakula na Kilimo wa Ujerumani Bw. Michael Stubgen akipata maelezo kutoka kwa Bi. Victoria Gowele  mmoja wa watafiti katika mradi huo wa namna walivyowafundisha wanafunzi namna ya kuwa na bustani ya matunda. (Picha na Gerald Lwomile)

Naye Dk. Hadijah Mbwana mtafiti katika mradi huo amesema kuwa SUA kupitia mradi huo imewawezesha wananchi wa kijiji cha Chinoje mkoani Dodoma kuwa na uhakika wa maji safi na salama kwa kufufua kisima cha maji ambacho kitakuwa na uhakika wa kuhudumia vijiji viwili.

Wakielezea kwa undani shughuli za mradi, wanafunzi wa shahada za uzamivu waliofadhiliwa na mradi huo Bi Nyamizi Bundala na Bi Victoria Gowele wamesema kwa pamoja kuwa mchakato shirikishi wa kuchagua njia bunifu kutekeleza fursa za lishe kupitia kilimo mseto na elimu ndio chachu ya mafanikio ya mradi huo.

 katibu mkuu akizungumza

Katibu Mkuu wa Wizara ya Chakula na Kilimo wa Ujerumani  Bw. Michael Stubgen akizungumza na wanakijiji  wa Chinoje  , kushoto aliyekaa ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Prof. Siza Tumbo. (Picha na Gerald Lwomile)
 
 Mradi huo uliotekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2016, hadi kukamilika kwake umefadhili masomo ya shahada ya uzamivu kwa wanafunzi wawili na shahada ya uzamili kwa wanafunzi wanne kwa SUA pekee.

mashine ya kukaushia mbogamboga

Moja ya mashine ya kukaushia mbogamboga ambayo mradi wa SCALE-N umeipeleka kwa wanakijiji kwa ajili ya mafunzo. (Picha na Gerald Lwomile)

Jengo la kituo hicho cha lishe na biashara na kisima kirefu cha maji vimefunguliwa rasmi  na Waziri wa Kilimo na Chakula wa Ujerumani Bw. Michael Stubgen hivi karibuni.

jengo chinoje

Jengo lililojengwa na mradi wa SCALE-N kijijini Chinoje (Picha na Gerald Lwomile)

 

SUA yatoa milioni 20 kuboresha SUAFM 101.1 na SUATV

Na Gerald Lwomile

Bodi ya Taasisi ya Elimu ya Kujiendelea Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA imeipongeza menejimenti ya Chuo hicho kwa kuendelea kufanya maboressho makubwa katika Taasisi hiyo ikiwemo vyombo vya habari vya SUA yaani SUATV na SUAFM 101.1.

Mtangazaji Studio

Mtangazaji wa Kipindi cha Kapu la Leo Farida Mkongwe akiwa studio kuendesha kipindi hicho

Akizungumza katika kikao cha Bodi hiyo kilichoketi Machi 8, Mkurugenzi wa Taasisi hiyo ambaye pia Mwenyekiti wa Bodi hiyo Prof. Dismas Mwaseba amesema maboresho hayo yanayofanywa na menejimenti ya SUA yatasaidia utendaji wa Taasisi hiyo.

Amesema tayari Taasisi hiyo imefanya ukarabati mkubwa uliogharimu zaidi ya shilingi Milioni 80 wa hosteli yake iliyopo chuoni hapo na hivi sasa inaweza kupokea wageni ambapo amesema kwa sasa wanatoa kipaumbele kwa wanafunzi wa Shahada ya Uzamili na Umahiri wanaotoka nje ya nchi.

Ameongeza kuwa hii ni baada ya kupokea ushauri kutoka kwa Makamu wa Mkuu wa Chuo hicho Prof. Raphael Chibunda katika kuhakikisha wanafunzi wanaotoka nje ya nchi hawapati shida ya maeneo ya kukaa na usalama wao kwa ujumla.

Aidha Bodi hiyo imeupongeza uongozi wa SUA kwa kutoa karibu Shilingi milioni 20 kuimarisha vituo vyake vya habari vya Redio SUAFM 101.1 na Televisheni SUATV ikiwa ni pamoja na kuhakikisha vituo hivyo vinakuwa hewani wakati wote ambapo kwa sasa wakati umeme unapokati katika eneo la Chuo vituo hivyo hushindwa kuwa hewani.

 

WAZIRI LUGOLA APIGA MARUFUKU POLISI JAMII KUKAMATA BODABODA, ASKARI POLISI KUKAMATA VYOMBO VYA MOTO BILA KUVAA SARE ZA JESHI

Na:Tatyana Celestine

 
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amepiga marufuku Polisi jamii kukamata bodaboda zinazofanya makosa ya usalama barabarani nchini.
 
Pia Waziri huyo amepiga marufuku polisi wa usalama barabarani kukamata vyombo vya moto wakiwa hawajavaa sare za Jeshi.
image 2019 03 08
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati), akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Morogoro, leo. Lugola yupo Mkoani humo kwa ziara ya kikazi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 
 
Akizungumza na mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Shule ya Msingi Mafisa, Kata ya Mwembesongo, mjini Morgoro, jana, Lugola alisema Polisi Jamii hawana ujuzi wa kijeshi wa ukamataji wa bodaboda hivyo kuendelea kuifanya kazi hiyo ni kuwanyanyasa wananchi.
 
“Nimepata malalamiko mengi ninapofanya ziara zangu hapa nchini, wengi wanawalalamikia Polisi Jamii kuwaonea, kuwaomba rushwa na kuwakamata pasipofuata utaratibu unaotakiwa kijeshi, hapa Morogoro pia, katika mkutano huu wa hadhara mnayasema yale yale, sasa natangaza kuanzia leo, marufuku Polisi Jamii kukamata bodaboda,” alisema Lugola. 
 
Waziri Lugola pia alipiga marufuku baadhi ya Polisi wa Usalama barabarani ambao wenye tabia ya kutovaa sare za Jeshi na kuingia barabarani au mitaani na kuyakamata magari na bodaboda.
Lugola alisema lazima polisi wafate sheria za usalama barabarani hasa wanapokamata magari yanayofanya makosa, uvaaji wa sare za Jeshi ni muhimu na unapaswa kufutwa.
 
image 2019 03 08
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akimfafanulia jambo Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Regina Chonjo (katikati), mara baada ya kumaliza Kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa huo, SACP-Wilbroad Mutafungwa.  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 
Waziri Lugola aliongeza kuwa, bodaboda au vyombo vingine vya moto, zinazovunja sheria za usalama barabarani zinapaswa kukamatwa bila kuwaonea huruma, ila ni kosa Polisi kuwanyanyasa vijana hao ambao wanapata ridhiki kupitia biashara hiyo.
 
“Mnapaswa kukamata hizi bodaboda zinapofanya makosa, tabia ya kukurupuka huku mkitafuta fedha zisizo halali, huko ni kuwaonea waendesha bodaboda,” alisema Lugola.
 
Lugola alifafanua kuwa, bodaboda zinazotakiwa kuwepo kituo cha polisi ni zile zilizopo katika makundi matatu ambayo ni Bodaboda zilizohusika kwenye uhalifu, zilizotelekezwa au zilizookotwa na zilizohusika katika ajali.
 
“Bodaboida hizo ndizo zinapaswa kuwepo vituoni, lakini kuziweka bodaboda ambazo hazipo katika makundi hayo, napiga marufuku na hii nataka Polisi nchi nzima munielewe,” alisema Lugola.
Pia Lugola aliwataka waendesha bodaboda mjini Morogoro na Tanzania kwa ujumla wafate sheria za usalama barabarani zikiwemo kuvaa kofia ngumu, kutokubeba abiria zaidi ya mmoja na pia wakiendesha wanapaswa kuwasha taa. 
 
Lugola ameanza ziara yake ya siku tatu mkoani humo akitembelea Wilaya za Morogoro, Mvomero, Kilosa na Gairo akisikiliza kero za wananchi pamoja na kufuatilia maagizo yake aliyoyatoa kwa vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya Wizara yake. 
 
Lugola mwaka jana alitoa maagizo kwa makamanda wa mikoa nchini ambayo ni dhamana zitolewe saa 24 katika vituo vyote vya polisi nchini, na pia kupiga marufuku tabia ya baadhi ya Polisi kubambikizia kesi wananchi, na pamoja na agizo la pikipiki zote zilizopo vituoni ziondolewe.
 
Waziri Lugola amemaliza ziara Wilaya ya Morogoro na leo ataanza ziara yake katika Wilaya ya Movemero, na Machi 10, 2019 atamalizia Wilaya ya Gairo ambapo katika Wilaya hizo pia atazungumza na wananchi pamoja na watumishi waliopo ndani ya Wizara yake ambao ni Jeshi la Polisi, Idara ya Uhamiaji, Jeshi la Magereza, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, pamoja na Idara ya Probesheni.
 
 
 

Prof. Robinson Mdegela: Kufikia mwaka 2050 kutakuwa na ongezeko la vifo kutokana na matumizi mabaya ya vyakula

Na:Vedasto George

Kutokana na kuwepo kwa  ongezeko kubwa la magonjwa ya wanyama,mimea  na binadamu  nchini  wadau kutoka Vyuo Vikuu vinavyofundisha  maswala ya  Afya  ya wanyama na binadamu  ikiwemo Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA)  wamepewa mafunzo ya jinsi   watakavyo  fundisha  somo la Afya Shirikishi (Afya  moja) kwa wanafunzi kuanzia ngazi ya cheti na astashaada.

afya moja 2

Mwezeshaji Mkuu kutoka  Chuo Kikuu cha Afya  Muhimbili (MUHAS) Prof. Japhet Killewo(Kushoto) pamoja na Msimamizi Mkuu wa shuguli za mtandao wa Afya Shirikishi (AFYA MOJA)Prof Robinson Mdengela  (Kulia) wakifuatilia namna mafunzo hayo yanavyoendelea.(Picha na Vedasto George).

 

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo Msimamizi Mkuu wa shuguli za mtandao wa Afya Shirikishi (AFYA MOJA)Prof Robinson Mdengela Amebainisha kutokana na Bara la Afrika inatarajiwa kufikia mwaka 2050 kutakuwa na ongezeko la vifo kutokana na matumizi mabaya ya vyakula pamoja na kutumia viuwatilifu kwenye mbogamboga hivyo itapelekea magonjwa kama Kansa na Shinikizo la damu.

Aidha amesema kuwa mafanzo hayo yanayotolewa yatakuwa na faida kwa kila eneo hasa vijijini kwani walengwa wa mafunzo hayo ni wale waishio vijijini ambapo maafisa ugani wenye elimu ya afya ngazi ya cheti na astashaada ndio wanaohudumu vijijini  hivyo  itakuwa rahisi kuweza kufikisha elimu hiyo kirahisi kwa walengwa.

afya mojaWashiriki katika mafunzo ya Afya Shirikishi (Afya moja) wakifuatilia mafunzo hayo yaliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA.(Picha na Vedasto George).

 

Nae Mwezeshaji Mkuu kutoka  Chuo kikuu cha Afya  Muhimbili (MUHAS) Prof. Japhet Killewo  amesema kuwa  kutoka mwaka 2010 wamekuwa wakitoa mafunzo kwa  wadau wanaofundisha maswala ya  Afya  ya wanyama,mimea  na binadamu kwa lengo la  kuona jinsi gani  wanaweza kukabiliana  na changamoto itokanayo na magonjwa ya mlipuko yanayo ambukiza ikiwemo Ebola.

Shabani Mshamu kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) na Selestina Amos kutoka Wakala wa  mafunzo ya Afya ya Mifugo na uzalishaji (LITA) ni baadhi ya washiriki katika mafunzo hayo wakaeleza jinsi watakavyo tekeleza mafunzo kwa vitendo katika maeneo yao ya kazi.

Serikali yatakiwa kushirikiana na wajasiriamali kutatua changamoto zinazowakabili

Na, Catherine Mangula Ogessa

Katika maisha changamoto ni sehemu ya maisha ambayo mtu hupitia katika kuelekea  mafanikio. Wakristu wanaamini kuwa katika maisha hakuna Pasaka pasipo  Ijumaa kuu. Maneno haya yakimaanisha kuwa, daima mtu lazima apitie magumu ili kuweza kufikia kwenye mafanikio. Kauli hii inajidhihirisha ukisoma kwenye maandiko ya  Biblia takatifu katika kitabu cha  Marko 15:34, 37. Marko 16:6, Mathayo 28:5,6.

3.PROFPROF. ESRON KARIMURIBO akifungua mkutano wa wajasiriamali picha na Vedasto George

Inawezekana hata wewe ni mmoja wa watu ambao wamekutana na changamoto katika maisha, lakini hili sio kusudio la ninachotaka kusema katika Makala haya bali ninachotaka kusema ni changamoto wanazokutana nazo wajasiriamali katika kufikia mafanikio kwa yale wanayotamani kuyafanya. Kwanza kabisa msomaji wa Makala haya nikukumbushe kuwa  kila jambo lina changamoto zake, ujasiriamali nao unachangamoto zake nyingi na ni wazi kuwa kinachoweza kuzitofautisha  ni  chanzo cha hizo changamoto na namna  ambavyo mtu anaweza kuzitatua pindi zinapojitokeza . 

 2.Bi.Peace mushi mjasirialiamali picha na Vedasto georgeBi.Peace Mushi mjasirialiamali.( picha na Vedasto George.)

Wajasiriamali walio wengi huzitaja miongoni mwa changamoto ambazo zinawakabili kwenye shughuli zao kuwa ni pamoja na ukosefu wa mitaji, uhakika wa masoko na nyingine nyingi. Hivi karibuni Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kupitia kituo chake kinacho shughulika na masuala ya jinsia ambacho kinaratibu mpango wa kuendeleza na kuwawezesha vijana na wanawake wajasiriamali wa Tanzania, Kenya na Uganda, hivi karibuni kulikuwa na warsha iliyolenga kubadilishana uzoefu na uelewa kwa wajasiriamali ambao wamenufaika na ufadhili wa kwenda kujifunza nchini Marekani ambapo Michingan State University ndiyo wanaotekeleza mpango huo.

Katika warsha hiyo washiriki waliweza kueleza changamoto ambazo wanakutana nazo katika ujasiriamali wao ambazo ni pamoja na ukosefu wa pesa za kuweza kuendesha shughuli zao, ukosefu wa uwezeshwaji kutoka serikalini lakini pamoja na ushirikiano kutoka kwa jamii.

4.Bi. Enikia Wilfred Bisanda akiwasilisha mchango katika warsha Picha na Vedasto George.1Bi. Enikia Wilfred Bisanda akiwasilisha mchango katika warsha Picha na Vedasto George

Wakibadilishana uzoefu washiriki hao walibainisha kuwa miongoni mwa mambo ambayo ni changamoto kwao waliyoyabainisha kutoka nchini Tanzania ambayo ni tofauti na Marekani, miongoni mwa wanufaika wa ufadhili wa kwenda kujifunza nchini Marekani ni Bi. PEACE MUSHI ambaye ni mjasiriamali katika kilimo na ufugaji alisema kuwa miongoni mwa mambo ambayo wameyaona nchini Marekani ni pamoja na Serikali kuwa karibu zaidi na wajasiriamali , ambapo kwa hapa Tanzania ni tofauti.

“ Marekani serikali imekuwa ikishirikiana na wajasiriamali katika kupanga mambo yao kuhusu shughuli za kijasiriamali, kuwapatia wataalam, kusaidia katika kutangaza, namna ya kupata wateja wa bidhaa zao, pamoja na kuweka mipango yao”, alisema Bi. Peace Mushi.

Katika kukabiliana na changamoto washiriki hao waliiomba Serikali kukaa karibu na wajasiriamali ili waweze kujua changamoto zinazo wakabili na baadae kuweza kuangalia njia ya kuzitatua changamoto hizo kwani changamoto nyingi ambazo wajasiriamali wamekuwa nazo inawezekana hazifahamiki kwa serikali.

5.Daktari John Jeckoniah1Daktari John Jeckoniah.

Kauli hiyo imetolewa na wanufaika wa mpango wa kuwaendeleza na kuwawezesha vijana na wanawake wajasiriamali wa Tanzania, Kenya na Uganda ambao walipata ufadhili wa ziara ya mafunzo kwa wajasiriamali kwenda wiki nne za mafunzo nchini Marekani.

Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uzamili, Utafiti, Uhaulishaji wa Teknolojia na Ushauri wa Kitaalam kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA  PROF. ESRON KARIMURIBO aliwataka washiriki wa warsha hiyo kuhakikisha wanajifunza njia za namna ya kujiajiri wenyewe lakini pia kutafuta namna ya kuzibadilisha changamoto kuwa fursa.

“Warsha hii ilete manufaa kwenu kwa kila upande kuhakikisha inawaunganisha wajasiriamali na wabunifu ili kila upande uweze kujifunza kwa mwenzake na hatimaye mjifunze namna ya kuweza kupata ajira”, alisema Prof. Esron Karimuribo.

1.Washiriki wa warsha ya wajasiriamali picha na Vedasto GeorgeWashiriki wa warsha ya wajasiriamali picha na Vedasto George

Pamoja na changamoto hizo lakini pia watu wengi wamekuwa hawawezi kuthubutu kufanya jambo wakihofia kushindwa lakini Bi.  Enikia Wilfred Bisanda ambaye ni miongoni mwa wanufaika wa ufadhili huo wa ziara ya mafunzo aliwataka vijana pamoja na wanawake kuacha woga wa kujihusisha kwenye masuala ya biashara pamoja na ujasiriamali kwa kuhofia  changamoto ambazo zinaweza kujitokeza  na badala yake wathubutu kufanya kile walichonacho.

“Vijana na wanawake ni muhimu wahakikishe wanathubutu kwani wakifanya hivyo watajua namna ya kukabiliana na changamoto, lakini pia itawasaidia kujua wafanye nini ili kuweza kuzalisha kulingana na mahitaji ya soko” , alisema Bi. Enikia Wilfred Bisanda.

 

Katika hatua nyingine Bi. Sanda amewataka kuhakikisha wanakuwa wanashiriki semina pindi wanaposikia kuna fursa hizo kwani semina hizo zitawajenga katika masuala ya ujasiriamali

Awali akielezea washiriki wa mpango huo mratibu wa mpango huo kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA ambapo wao wamekuwa wakiratibu na watekelezaji wake wakiwa ni Michingani State University Daktari John Jackonare ambaye pia ni mratibu katika kituo cha masomo ya jinsia amesema kuwa kwanza kabisa mpango huo unashirikisha vyuo vikuu vitatu ambavyo ni SUA cha Tanzania, Nairobi cha Kenya pamoja na Kyambogo cha nchini Uganda.

NDAMA ALIYEZALIWA NA PUA MBILI AMEFIKISHWA SUA KWA MATIBABU

Na Amina Hezron,Morogoro

Ndama wa ajabu mwenye pua mbili ameezaliwa jana katika Gereza la Mbigiri wilayani Mvomero na kufikishwa leo katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Akizungumza na SUAMEDIA, Rasi wa Ndaki ya Tiba ya Mifugo na Sayansi za Afya Prof. Donald Mpanduji amesema kuwa walipokea taarifa ya kuzaliwa kwa ndama huyo kutoka katika gereza la Mbigiri na kuagiza ndama huyo kuletwa katika Kliniki ya Mifugo ambayo pia ni ya Rufaa chuoni hapo.

picha tatu

Mkuu wa Rasi wa Ndaki ya Tiba ya Mifugo na Sayansi za afya Prof. Donald Mpanduji wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) akitoa maelezo juu ya ng'ombe wa ajabu aliyefikishwa katika Kliniki ya Rufaa ya wanyama SUA.

 

Prof. mpanduji amesema lengo la kuagiza ndama huyo kuletwa ni kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi ambapo pia amesema tatizo hilo ni la kawaida kwa mnyama kutokea.

Prof. Mpanduji amefafanua kuwa hii ni mara ya kwanza kwa tatizo kama hilo kuripotiwa katika kliniki hiyo hivyo ndama huyo kwa sasa atafanyiwa uchunguzi ili iweze kutambulika ukubwa wa tatizo lake hasa katika njia ya mfumo wa hewa na chakula.

picha ya Ndama

Ndama wa ajabu mwenye pua mbili aliyezaliwa katika Gereza la Mbigiri wilayani Mvomero amefikishwa katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kwaajili ya uchunguzi zaidi.

 

Aidha Prof Mpanduji amewataka wafugaji wanapokutwa na matatizo kama hayo kwa wanyama kutokimbilia kuhusisha na Imani za kishirikina na kuripoti katika sehemu za taaluma ikiwemo katika Kliniki hiyo iliyopo katika Ndaki ya Tiba ya Mifugo na Sayansi za Afya kwa ajili ya ushauri wa kitaalamu na kuwataka pia wafugaji kufata ufugaji bora wa wanyama.

MRADI WA RIPAT SUA WAWAWEZESHA WAKULIMA MOROGORO

Na: Bujaga I. Kadago

Wanachuo wanaosomea shahada ya usimamizi katika  wa miradi chuoni SUA wameridhika na matokeo ya mfumo shirikishi wa kuleta mapinduzi ya kilimo RIPAT baada ya kujionea shughuli za kilimo na ufugaji katika wilaya ya Mvomero.

kakaaa

Mwenyekiti wa Kikundi cha Twawave Bwana Jerome Jacob kutoka Kijiji cha Mnyanza Kata ya Tangeni akifafanua jambo kwa wanafunzi wanaosomea Shahada ya Uzamili ya Usimamizi katika  wa miradi SUA.

Ziara hiyo ya Wananchuo wa SUA  kutembelea vijiji vya Changarawe,Tangeni,Kauzeni na Mnyanza katika Wilaya ya Mvomero na Manispaa ya Morogoro ilikuwa sehemu ya mafunzo kwa vitendo baada ya kusoma nadharia ya mfumo huo wa RIPAT

kijanaaMhadhiri wa SUA Dkt. Goodluck Masawe  aliyeambatana na kundi la kwanza la wananfunzi hao walio nyuma yake akizungumza na wanakikundi hawapo pichani.

Mmoja wa wanachuo hao Bwana Mrutu Ally amesema mfumo huo wa RIPAT ni rahisi na sahihi katika kuhamasisha teknolojia kutoka kwa watafiti na kuzipeleka kwa wakulima wadogo vijijini ambapo matokeo yake ni Dhahiri kwani mikungu ya migomba ni mikubwa.

mgomba 

Shamba la migomba la kikundi cha NURU katika Kijiji cha Changarawe Mvomero.

Aidha wanachuo hao wameridhishwa na mfumo wa uanzishwaji vikundi, uchaguzi wa aina ya zao wanalopenda kulilima na pia mfumo wa mafunzo ya vitendo katika kufundishwa teknolojia mpya za kilimo na ufugaji wanazopelekewa.

 

VIONGOZI WAANDAMIZI WA CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA ILLINOIS MAREKANI WATEMBELEA SUA

Na: Bujaga I. Kadago

Viongozi waandamizi kutoka Chuo Kikuu cha Illinois na wengine kutoka Benki ya chakula ya Midwest ya nchini Marekani wamefanya ziara ya kikazi katika Chuo kikuu cha  Sokoine cha kilimo SUA ili kubaini fursa na maeneo ya ushirikiano baina ya taasisi hizo.

kipimoMtekinika Mwandamizi Bw. Jackson Bagilisha akitoa maelezo kwa wageni kutoka Chuo Kikuu cha Taifa cha Illinois  nchini Marekani kuhusiana na Utafiti wa ubora wa afya ya mbegu wakati wa Ziara yao Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA.(Picha na Tatyana Celestine)

Ujumbe huo kutoka Chuo cha Illinois ukiongozwa na Dr. Larry Dietz ambaye ni Rais wa Chuo hicho na Bw.Ralf Endress  kutoka Benki ya Chakula ya Midwest, umepokelewa na mwenyeji wao Makamu wa Mkuu wa chuo cha SUA Prof. Rafael Chibunda pamoja na  Viongozi wengine waandamizi wa chuo.

Akizungumza kwa niaba ya  Makamu wa Mkuu wa chuo, Mhadhiri Mwandamizi Idara ya Teknolojia ya Chakula na Sayansi ya Lishe na Mlaji Dr. Kisa Kulwa amesema ujumbe huo ni muhimu kwani utafungua fursa katika maeneo mbalimbali ikiwemo Nyanja za utafiti,ufundishaji na ubadilishanaji wa wakufunzi na wanafunzi baina ya vyuo hivyo kwa lengo la kupata uzoefu na changamoto mpya.

 

mkonoWageni kutoka Chuo Kikuu cha Illinois cha nchini Marekani wakielezea faida waliyoipata kutembelea Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA. (Picha na Tatyana Celestine)

Aidha Dr. Kisa amesema kuwa  Chuo kinatambua mahitaji ya jamii hususani katika kilimo hivyo chuo kinaendelea kufanya tafiti mbalimbali ili kutoa ufumbuzi wa changamoto zinazoikabili jamii.

shambaaMtekinika Mwandamizi Bw. Jackson Bagilisha akielezea jinsi teknolojia ya uzalishaji wa migomba kwa wingi inavyofanyika na hatua zake katika Kitalu nyumba kimojawapo katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA).(Picha na Tatyana Celestine)

Ziara hiyo imekamilika Alhamis  Jan 31,2019 kwa majadiliano ya maswala mbalimbali pamoja na kutembelea baadhi ya idara ikiwemo Idara ya Sayansi ya Uhandisi na Teknolojia na  Kituo cha Utafiti wa Ubora na Afya ya mbegu.

WAKULIMA WATAKIWA KUITUMIA MAABARA YA UDONGO YA SUA ILI KULIMA KWA UFANISI

Na: Farida Mkongwe

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeahidi kuendelea kushirikiana na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA  katika kuhakikisha chuo hicho kinatimiza majukumu yake ipasavyo hasa yale yanayohusu kilimo.

nyambiMkuu wa Idara ya Sayansi ya Udongo Dr. Nyambilila Amor akitoa maelezo kwa Naibu katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe, Makamu wa Mkuu wa Chuo Prof. Raphael Chibunda na Naibu Makamu wa Mkuu wa Chuo Taaluma Prof. Peter Gillah wakati wa ziara ya Naibu Katibu huyo yenye lengo la kujionea namna maabara ya udongo SUA  inavyofanya kazi.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa James Mdoe wakati alipofanya ziara katika Maabara ya Udongo iliyopo Idara ya Sayansi ya Udongo SUA kwa lengo la kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa katika maabara hiyo.

Prof. Mdoe amesema serikali inashirikiana na vyuo vikuu nchini ikiwemo SUA katika kuhakikisha vyuo hivyo vinatimiza majukumu yake na tayari makubaliano yameshafanyika ya kuangalia namna ya kuvisaidia vyuo hivyo.

mlee

“Nimefika na kujionea maabara nzuri ya udongo namna inavyofanya kazi sisi tumejipanga kuwasaidia jambo la msingi nawashauri wakulima wazitumie maabara hizi ili waweze kulima kilimo chenye tija kwa sababu ili kuzalisha kwa ufanisi ni lazima kujua aina ya udongo unaohitajika”, alisema Prof. Mdoe.

Naibu Katibu Mkuu pia ametembelea nyumba za uatamizi katika mradi unaoendeshwa na SUA kwa kushirikiana na shirika la PASS na kuwapongeza SUA pamoja na vijana waliojitokeza kushiriki katika mradi huo ambao utawawezesha kupata maarifa kuhusu shughuli mbalimbali zinazohusu kilimo.

Kwa upande wake Makamu wa Mkuu wa Chuo Prof. Raphael Chibunda amemueleza Naibu Katibu Mkuu changamoto kubwa iliyopo katika maabara ya Udongo kuwa ni upungufu wa wataalamu wa maabara na kwamba katika kukabiliana na changamoto hiyo chuo kimeajiri wataalamu wawili kwa malipo ya ndani jambo ambalo limepongezwa na Prof. Mdoe.

 

SUA imewakutanisha wadau wa mnyororo wa thamani wa wakulima wa Alizeti na wafugaji wa kuku

Na: Calvin Gwabara

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kwa kushirikiana na wadau wengine kimewakutanisha wadau wa mnyororo wa thamani wa wakulima wa Alizeti na wafugaji wa kuku kwa lengo la kujadili changamoto zinazozikabili sekta hizo na kuweka mikakati ya kuzitatua ili kuongeza tija kupitia mnyororo wa thamani.

mbeleeWadau wa Mnyororo wa Thamani  wa zao la Alizeti na Ufugaji kuku wakiwa kwenye mkutano wa wadau wote kujadili namna ya kujenga mashirikiano .   (Picha na Calvin Gwabara)

Akizungumza nje ya mkutano huo Mratibu wa Programu ya Building Stronger Universities  BSU kwenye kitengo kinachosimamia mnyororo wa thamani wa mazao ya kilimo Dkt. Daniel Ndyetabula Kutoka Shule Kuu ya Uchumi Kilimo na Stadi za Biashara amesema kuwa hivi sasa wanafanya utafiti wa kuangalia mnyororo wa thamni na namna ambavyo wadau wanaweza kushirikiana.

Amebainisha kuwa wameitisha mkutano huo kwa kuwajumuisha wadau wanaofanya kazi kwenye mnyororo wa thamanii wa kuku na zao la alizeti ili  kuona namna wanavyoweza kushirikiana katika kujadili namna bora za kutatua changamoto za mnyororo wa thamani.

unenee (Picha na Calvin Gwabara)

Amefafanua kuwa matarajio yao makubwa  yalikuwa ni kufikia maazimio ya namna bora ya kushirikiana kati ya watafiti na wadau na kupitia mkutano huo  wamefanikiwa kutengeneza mpango bora wa mashirikiano ambao utatoa dira ya namna ya sekta hizo zitakavyoweza kutoa tija inayokusudiwa.

“Vigezo vilivyotumika  kuchangia mnyororo wa thamani wa alizeti na kuku ni kutafuta sekta ambazo zinaweza kutoa ajira kwa watu wengi ndio maana tukaona tuanze na kuku na alizeti kwa  kuwa sehemu hizo zina uwezo wa kutoa ajira nyingi kuliko zingine”, alisema Dkt.Ndyetabula.

Kwa upande wake Julie Mkambaita ambaye ni Afisa Mtendaji wa Chama cha Wasindikaji wa Alizeti mkoa wa Manyara na Prince Mosha amesema kuwa Kilimo cha alizeti kinakabiliwa na changamoto nyingi hususani mbegu bora kulingana na maeneo hivyo watafiti kuamua kusimamia zao hilo kutasaidia kupatikana kwa  ufumbuzi wa changamoto hiyo.

muzungu (Picha na Calvin Gwabara)

Naye Mwenyekiti wa Ushirika wa Wafugaji wa Kuku mkoa wa Morogoro amekishukuru Chuo Kikuu cha Sokoine na wadau wengine kwa kuitisha mkutano huo ambao umeweka mikakati ya namna ya kuboresha na kuinua sekta hiyo inayokuwa kwa kasi.

Amesema kupitia ushirikiano huo wafugaji wa kuku wataweza kupata taarifa muhimu za masoko na kupata mbinu bora za ufugaji kutoka kwa watafiti hao tofauti na hivi sasa ambapo kila mtu anaingia kwenye ufugaji bila kujua undani wa biashara hiyo.

 

Jamii imeshauriwa kuwa waangalifu katika kuepuka  ajali zinazoweza kujitokeza majumbani kutokana na wanyama wapya wawafugao

Na: Josephine Mallango

Jamii imeshauriwa kuwa waangalifu katika kuepuka  ajali zinazoweza kujitokeza majumbani hasa wanapoleta wanyama wapya kwa kuwa wanyama hao wanakuwa hawajazoeana na wanadamu na wanyama wengine waliopo katika eneo hilo.

Ushauri huo umetolewa na Daktari Mkazi  katika Hospital ya Rufaa ya Wanyama SUA Dk. Isaac Kashoma  wakati wakiwa katika maandalizi ya kumfanyia upasuaji wa mguu  mnyama aina ya mbwa aitwaye Bobi aliyejeruhiwa vibaya na mbwa wengine wenyeji.mbwaa

 Mbwa aliyejeruhiwa na Mbwa wenzie akifanyiwa upasuaji mara baada ya kufikishwa katika Hospital ya Rufaa ya Wanyama SUA 

Mbwa huyo jike anasadikiwa kuwa na umri wa kati ya miezi 4 au 5  ambaye ana majeraha makubwa shingoni unayoweza kusema amekatwa kwa mapanga au amenusurika kuchinjwa huku akiwa amevunjika mguu wa mbele wa kushoto ambaye alishambuliwa na mbwa wenzake.

Akisimulia mkasa huo daktari mkazi Isaac Kashoma amesema walimpokea mbwa huyo siku ya jumatano iliyopita jioni akiwa na hali mbaya na ndipo walimlaza wodini na kuanza kumpa huduma ikiwepo ya dripu za maji na kupigwa X-Ray ambapo alifanyiwa upasuaji na sasa anaendelea vizuri.

shingoo

 

Katika hatua nyingine Dk. Kashoma amesema kwa sasa jamii imekuwa na mwamko wa kuhudumia wanyama wanaofungwa  majumbani tofauti na miaka ya nyuma kutokana na ongezeko la wanyama wanaotibiwa katika hospital ya rufaa ya SUA kuongezeka ikiwa ni kutoka mkoani morogoro na nje ya Morogoro ikiwemo jijini Dar es Salaam.

kidonda Mbwa aliyejeruhiwa na Mbwa wenzie akionekana mara baada ya  kufanyiwa upasuaji katika Hospital ya Rufaa ya Wanyama SUA 

 

Ameongeza kuwa  wafugaji wanaotibu wanyama ni wa hali zote na idadi kubwa ni watu wa kawaida na hasa watoto wanaoleta mbwa  wao katika utaratibu wa kawaida wa kuwaosha na chanjo siku ya jumamosi huku idadi inayofuata ni wale wenye kipato cha kati  wanaoleta mbwa wenye magonjwa ya kutibiwa na kuondoka na wengine ni wale wanaoleta mbwa kwa ajili ya kulazwa na upasuaji.

 

SUA ni moja kati ya vyuo vinavyotoa elimu bora ya masomo ya Sayansi Afrika na Duniani

Na: Joel Memba

Naibu wa Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Sokoine cha Kililmo SUA  Prof. Peter Gillah amewahakikishia wanafunzi waliochagua kujiunga na masomo ya shahada ya juu kuwa Chuo kitahakikisha kinawasaidia kufikia malengo katika mafanikio yao ya kielimu

Prof. Gillah amesema hayo katika siku ya ukaribisho na utambulisho wa kuyajua mazingira iliyofanyika katika ukumbi wa “New Lecture Theater”  uliopo Kampasi Kuu ya chuo hicho huku  ikihudhuriwa na wakuu Ndaki,Shule ya Uchumi Kilimo,Wakurugenzi mbalimbali wa Taasisi na Viongozi wengine wa Chuo.karimuribo

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma Prof. Peter Gillah akijadili na Mkurugenzi wa Uzamili,Utafiti na Uhaulishaji wa Teknolojia na Ushauri SUA Prof. Ezron Karimuribo  

 

Prof. Gillah amesema kuwa  SUA ni moja kati ya vyuo vinavyotoa elimu bora ya masomo ya Sayansi Afrika na Duniani hivyo wanafunzi waliopata fursa ya kuchaguliwa ni muhimu wafuate kanuni, sheria na taratibu za kimaadili za Chuo ili kufikia malengo yao kitaluma na kimaisha.

 

washiriki

Viongozi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA pamoja na wanafunzi walioshiriki katika siku ya ukaribisho na utambulisho wa kuyajua mazingira iliyofanyika katika ukumbi wa “New Lecture Theater”  uliopo Kampasi Kuu.

Prof.Gillah amewataka wanafunzi hao kushiriki kikamilifu katika michezo,dini na maswala mengine ya kijamii bila kuathiri lengo la msingi la kitaaluma na kusisitiza kuwa huduma za kimatibabu,maabara na maktaba kuwa zimeboreshwa kwa kiwango kikubwa.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi Mkurugenzi wa Uzamili,Utafiti na Uhaulishaji wa Teknolojia na Ushauri Prof. Ezron Karimuribo amewakumbusha wanafunzi waliopokelewa kujiunga na masomo ya shahada ya juu kutambua wajibu wao binafsi, kwa familia,Taasisi na Taifa na kuepuka mambo yanayoweza kupelekea kufukuzwa chuoni.

group

Katika picha ya pamoja Naibu wa Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma SUA Prof. Peter Gillah wa tano kutoka kulia mstari wa mbele, Viongozi na Wanafunzi katika siku ya ukaribisho na utambulisho wa kuyajua mazingira iliyofanyika katika ukumbi wa “New Lecture Theater”  uliopo Kampasi Kuu

Wanafunzi SUA wajengewa uzoefu katika Sekta ya Utalii

Wanafunzi wa mwaka wa kwanza hadi wa tatu wanaosoma Shahada ya Utalii katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA wamepanda mlima Uluguru hadi katika eneo la Morning Site linalomilikiwa na Chuo hicho kwa lengo la kufanya mazoezi kwa vitendo na kujifunza mbinu za kuongoza watalii kwenye maeneo ya milima.

IMG 8302

Akiongea na SUAMEDIA Mkuu wa Idara ya Utalii na Mapumziko uishi Dkt. Agnes Sirima amesema kuwa idara hiyo imekuwa ikiwafundisha wanafunzi hao nadharia lakini pia huwawezesha kwenda katika maeneo ya kitalii ya aina mbalimbali kwa lengo la kupata uzoefu wa kutosha kabla hawajamaliza masomo yao na kuingia kwenye soko la ajira.

“Tunaposema utalii wa kupanda kwenye milima,shughuli za utalii, uongozaji watalii na ushirikishwaji wa jamii katika utalii na vitu vingine vingi katika sekta ya utalii lazima wanafunzi wajifunze kwa matendo, hivyo tumekuja nao kuwaonyesha kituo hiki cha Morning site ili wajue kipo kwenye idara yetu na waweze kukitumia kwa ajili ya mafunzo yao ya utalii” alisema Dkt. Sirima.

Amesema hii ni mara ya pili wamekuwa wanawapelekea wanafunzi katika eneo hilo lakini mwaka huu muitikio umekuwa mkubwa tofauti na mara zingine kwani wanafunzi na waalimu wao wamejitokeza kwa wingi na anaamini zoezi hilo litakuwa endelevu ili kusaidia kuwa na wahitimu bora.

Dkt. Sirima amesema hii inawajengea wanafunzi hao ambao wanatarajiwa kuja kuongoza watalii baadae kujiamini na kujua ni vitu gani vya muhimu wanapaswa kuvizingatia kabla ya kupanda mlima na watalii ikiwa ni pamoja na kufikia malengo ya mtalii kwa kumuandaa kikamilifu kwa mavazi,viatu na vitu vingine.

Akizungumzia safari hiyo mmoja wa wanafunzi wa kozi hiyo Irene Ibrahim amesema kuwa imemjengea uwezo wa kujua changamoto za upandaji milima na kujua mambo muhimu anayopaswa kufanya kabla ya kuanza kupanda mlima peke yake au pale atakapokuwa anaongoza mtalii katika kupanda mlima.

Amesema awali hakuzingatia aina za mavazi na viatu anavyotakiwa kuvaa wakati wa kupanda mlima hali ambayo imemfanya yeye na wanafunzi wengine kupanda mlima huyo kwa tabu kutokana na viatu na mavazi waliyovaa kutokuwa sahihi.

Kwa upande wake mratibu wa safari hiyo ya mafunzo Dkt. John Ngonja amesema kuwa kuna tofauti kubwa kati SUA na vyuo vingine nchini ambavyo vinatoa kozi ya utalii kwani chuo hicho kipo karibu na asili na hivyo kutoa fursa nzuri kwa wanafunzi kufanya mazoezi kwa vitendo na hivyo kuwa bora kuliko vyuo vingine.

Amesema msisitizo wa kozi wanazozitoa ni tofauti kwani wanajitahidi kuwafundisha utalii wa asili kwahiyo hiyo ni sehemu ya kutambua asili kwa kutoa kozi za Utalii wa Wanyamapori, Masoko na utalii, Uchumi,Ukarimu na Uongozaji Watalii.

Wakulima wa Kanda ya Mashariki wametakiwa kuchukua tahadhari

Na: Tatyana Celestine 

Wakulima wa Kanda ya Mashariki wametakiwa kuchukua tahadhari ili kuepukana na panya waharibifu wa mazao katika kipindi hiki cha mvua ambapo panya hao huleta uharabifu unaoweza kufikia asilimia 100.

Hayo yamesemwa Januari 17 na Prof Loth Mulungu kutoka Kituo cha Kudhibiti Viumbe Hai Waharibifu wakati akizungumza na SUAMEDIA ofisi kwake.

Prof. Mulungu amesema wakulima wengi hivi sasa wamenza kupanda mazao ya chakula lakini kama watachukua hatua za tahadhari wanaweza kujikuta wanapata hasara kubwa na kushindwa kunufaika na kilimo.

pori panyaPicha na Mtandao

Amesema ni muhimu wakulima waache kilimo cha mazoea ambacho huona kupata hasara ni jambo la kawaida kwani upo uwezekano wa kuzuia uharabifu kwa kusafisha mashamba yao mapema ikiwezekana mwezi mmoja kabla ya kupanda mbegu.

Aidha amebainisha kuwa wale ambao wamekwisha panda mazao yao mashambani pasi kufanya usafi na tayari panya wameanza kuvamizi wanatakiwa kuwaomba maafisa ugani wawape njia bora za kukabiliana na panya hao.

WANAFUNZI WANAOSOMA SUA WAKIWEMO WA KIGENI WABORESHEWA MAZINGIRA YA HOSTELI

Na Gerald Lwomile

Katika kuhakikisha usalama wa wanafunzi wa kigeni ambao husoma Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA, Chuo hicho kimefanya ukarabati wa moja ya Hosteli zilizopo chini ya Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza ICE  chuoni hapo jambo ambalo litasaidia kuhakikisha wanakuwa na maisha ya usalama muda wote watakaokuwa SUA.

IMG 8168

Makamu wa Mkuu wa Chuo Prof. Chibunda (wa pili kusoto) , na viongozi wengine wa Chuo wakipokea maelezo ya jengo lilikarabatiwa toka kwa Msimamizi wa Kitengo cha Huduma za Mikutano,Hosteli na Mgahawa katika Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza Dkt. Devotha Kilave wa kwanza kushoto.(Picha na Gerald Lwomile)

Akikagua ukarabati huo Makamu wa Mkuu wa Chuo hicho Prof. Raphael Chibunda amesema SUA itatoa kipaumbele kwa wanafunzi hao ambao wakati mwingine hujikuta wanakaa sehemu ambazo zinaweza kuhatarisha usalama wao na mali zao.

Akizungumzia ukarabati huo Msimamizi wa Kitengo cha Huduma za Mikutano,Hosteli na Mgahawa katika Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza Dkt. Devotha Kilave amesema ukarabati wa Hosteli hiyo umegharimu zaidi ya shilingi za kitanzania milioni 80 ukijumuisha samani mbalimbali ambazo zimewekwa katika hosteli hiyo.

JENGO

Muonekano wa Hostel iliyokarabatiwa katika Taasisi ya |Elimu ya Kujiendeleza (ICE. (Picha na Gerald Lwomile)

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza ICE Prof. Dismas Mwaseba amemshukuru Makamu wa Mkuu wa Chuo kwa kukubali Taasisi hiyo ifanye ukarabati huo ambao kwa kiasi kikubwa utasaidia wanafunzi na hasa watokao nje ya nchi kujifunza wakiwa katika mazingira mazuri.

Katika ukaguzi huo Makamu wa Mkuu wa Chuo Prof. Chibunda aliongozana na Naibu Makamu wa Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha Prof. Fredrick Kahimba, Mkurugenzi wa Uzamili, Utafiti na Uhaulishaji wa Teknolojia na Ushauri Prof. Esron Karimuribo na Mkuu wa Kitengo cha Uthibiti Ubora SUA Prof. Justin Urassa.

 

LUGOLA AMPA SIKU 30 MKUU WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI KUFANYA UKAGUZI TAASISI ZA UMMA NA BINAFSI NCHINI KAMA ZINA VIFAA VYA ZIMAMOTO

Na Felix Mwagara, MOHA-Biharamulo.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amempa siku 30 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kufanya ukaguzi taasisi mbalimbali za umma na binafsi nchini kuwa na vifaa vya zimamoto.

PIX 3Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na mamia ya wananchi wa Mji wa Biharamulo, Mkoani Kagera, leo. Lugola amempa siku 30 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kufanya ukaguzi taasisi mbalimbali za umma na binafsi nchini kuwa na vifaa vya zimamoto. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

 

Lugola alisema ukaguzi huo pia ulenge zaidi katika shule za msingi, sekondari na vyuo, vituo vya kutolea huduma za afya ili kuepukana na ajali zitokanavyo na vyanzo vya moto.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na mamia ya wananchi, ambao ulifanyika katika uwanja wa mpira Mjini Biharamulo, Mkoani Kagera, leo, Lugola alisema atafuatilia utekelezaji wa agizo lake kama litakua limefanyiwa kazi jinsi anavyotaka yeye.

PIX 2Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Kagera, Raymond Mwampashe, lipokua anamfafanulia jambo wakati Waziri huyo alipofika katika Gereza la Biharamulo mkoani humo kujua utendaji wa kazi wa Gereza hilo. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo, Saada Malunde. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

 

Pia Waziri Lugola amewaomba Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanatenga fedha za mapato ya ndani kununua vifaa za zimamoto katika taasisi za Serikali wanazoziongoza.

“Haiwezekani wanafunzi, wagonjwa katika zahanati mbalimbali au vituo vya afya wapate tatizo la ajali la moto halafu wakurugenzi na mameneja au wakuu wa taasisi hizo wakishindwa kuweka vifaa vya zimamoto licha ya kupokea fedha za kutolea huduma,” alisema Lugola.

PIX 1Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akitaka ufafanuzi wa jambo kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, (RPC) Revocatus Malimi (kushoto), wakati Waziri huyo alipopata malalamiko kuhusu ng’ombe za Mkazi wa Mji wa Biharamulo (kulia) kukamatwa na Polisi Wilayani Biharamulo. Hata hivyo, RPC alimfafanulia Waziri huyo kuhusiana na malalamiko hayo dhidi ya mifugo iliyokamatwa na Polisi na kuhifadhiliwa katika Gereza la Biharamulo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

 

Aidha, Waziri Lugola amezitaka taasisi za dini kuendesha ibada kwa kuhakikisha majengo yanasajiliwa na pia Miiskiti na Makanisa yasitumike kuhifadhi wahalifu wanaotumia migongo ya kuwa wachungaji na mashekhe kama mwavuli wa maadili mema bila uzalendo.

“Makanisa na miskiti itakayobainika ina malengo hayo, sitaona haya kuifutia usajili, na pia nawataka viongozi wa dini endapo migogoro inaibuka hakikisheni  mnaitatua wenyewe kwa amani,” alisema Lugola.

Pia Lugola alisisitiza akiitaka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kupitia upya usajili na utoaji wa vitambulisho vya taifa katika mikoa ya Kagera na Kigoma ili waweze kuwabaini  na kuwaondoa raia wa nchi jirani zinazoizunguka mikoa hiyo.

Subcategories

Page 1 of 38