SUASO NI DARAJA KATI YA MENEJIMENTI NA WANAFUNZI

Na:Alfred Lukonge

Rais wa serikali ya wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Bw.Peter Laurent Magembe amesema kuwa lengo kuu la Taasisi hiyo ni kuwa daraja kati ya wanafunzi na menejimenti ya chuo hicho kwenye kuwasilisha maslahi yao.

Bw.Magembe ambaye Taasisi hiyo anayoiongoza hujilikana kwa jina la  Sua Student’s Organization (SUASO) amesema hayo kwenye kipindi cha Tanzanite kinachorushwa hewani na redio SUA FM ambapo aliambatana  na makamu wake Bw.Malima Daniel.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

Pamoja na hayo pia Magembe amesema kuwa SUASO huwa inahakikisha inawajengea uwezo wanachama wake ambao ni wanafunzi ili waweze kuwa viongozi wa sasa na baadae.

Naye Bw.Malima Daniel akitoa neno kwenye kipindi hicho amesema kuwa ahadi yao kubwa wakati wakiomba  kura za uongozi ilikuwa ni kuwasaidia wanafunzi waweze kufanikisha malengo yao yaliyowaleta chuoni kwa kutoa kila aina ya msaada  ili kuweza kuwatatulia changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Aidha Daniel pia amebainisha kuwa kupitia SUASO wanajitahidi kuimarisha uhusiano na serikali za wanafunzi za vyuo vingine  ambazo maslahi yao yanarandana na SUASO.

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner