ASKOFU TELESPHOR MKUDE AITANGAZA PAROKIA YA MLIMA CARMEL KUWA PAROKIA KAMILI

  PICHA NA ALFRED LUKONGE   

ASKOFU TELESPHOR MKUDE AITANGAZA PAROKIA YA MLIMA CARMEL KUWA PAROKIA KAMILI

Na: ALFRED LUKONGE

Parokia ya   Bikira   Maria   ya  Mlima  Carmel  Kihonda  Maghorofani katika Manispaa ya Morogoro   imetangazwa   kuwa  Parokia   kamili   na  Mhashamu   Askofu  Telesphor  Mkude    wa   Jimbo  la  Morogoro   wakati  wa   sherehe   ya  kuadhimisha  miaka  mia tano  ya  kuzaliwa  mtakatifu   Teresia   wa   Havila.

Bofya kichwa cha habari kwa habari zaidi.......

 

Askofu   Mkude  ametoa  tangazo  hilo  wakati  akitoa   mahubiri   katika  sherehe  hizo ambako alikuwa   mgeni  rasmi  na  kutoa  angalizo  watu wanatakiwa  wamtii  Paroko wa  parokia hiyo  kwani  kwa  kufanya  hivyo  watakuwa   wamemtii  na  yeye  askofu pia.

 

Askofu   Mkude  ameongezea    mitume  iliyoachwa  na  Yesu   kueneza  Injili  walitumia  neno  Sharom  wakimaanisha  amani hili  wanadamu  tutoe   hofu  kwa sababu   hofu   inamaliza   nguvu  ya  mwanadamu  ndio  maana Mungu alimtoa  mwanae  wa  pekee  ili  atuondelee  wanadamu  hofu”.

 

Akimzungumzia  mtakatifu   Teresia wa  Havila   Askofu  Mkude   amemtaja  kama  ni  mwanamke  wa  kwanza  kutamkwa   mwalimu  wa  kanisa  kwenye   ngazi   za  kusali. Na kutoa  shukrani  za  dhati   kwa  shirika  la  Carmel   Tanzania  kwa kufanya  maadhimisho  haya mkoani Morogoro  ikiwa  ni  njia mojawapo  ya kuonyesha  mambo   mazuri  wanayofanya.

 

Ametoa  wito  kwa  familia  kuchukua   nukuu  ya  Mtakatifu   Teresia “ Mungu  pekee atosha” akisisitiza watu  wakiwa  kwenye  upendo  hakuna  mtu  atakayefikiria  kumpa  au   kumuomba  mwenzie  talaka.

 

 Akitoa   shukrani  zake   kwa   Askofu,   Paroko   wa  Parokia  hiyo   Padri   Vivian   Menezes  alimshukuru   sana   baba  Askofu  kwani ilikuwa  ni  kiu  yao  ya  muda  mrefu   kuwa  parokia   kamili   kutoka ya awali ya parokia teule.

 

Sikukuu  ya  kusherekea   miaka  mia  tano  ya Mtakatifu  Teresia     ilihudhuriwa   pia  na  Mkuu  wa  Shirika  la  Carmel   Tanzania Padri  Marlon   Rodrigues,  wakiwemo   mapadri  wote  wa  Shirika  hilo 

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner