VILEO MWISHO SAA SITA USIKU KUPISHA UCHAGUZI MKUU 2015- DKT. RUTENGWE

        

VILEO MWISHO SAA SITA USIKU KUPISHA UCHAGUZI MKUU 2015- DKT. RUTENGWE

Na:TATYANA CELESTINE 

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro  Dkt. Rajabu Rutengwe amewaagiza wamiliki wa Baa na Mamlaka  zinazotoa Leseni ya bidhaa za  vileo kuanzia tar 24-27 Octoba  2015 kufunga huduma ya baa kuanzia saa sita usiku na kutouza vileo kama viroba bila kuzingatia miiko ya biashara hizo kwa kupuuza agizo hilo kutapelekea uvunjifu wa Amani siku ya uchaguzi  ya tar 25 Octoba

Bofya kichwa cha habari kwa habari zaidi.......

 Dkt. Rutengwe amesema hayo alipoitisha Mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake leo ili kuwajulisha hari ya maandalizi na namna Serikali ilivyojipanga kusimamia kikamilifu zoezi la upigaji kura ambapo wananchi wataweze kuendelea  na maisha yao ya kawaida baada ya Uchaguzi

Aidha Mkuu wa Mkoa huyo ameitaka Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania( TFDA) kufuatilia kwa ukaribu mienendo ya wanaofanya biashara hizo ili wanapokiuka kuchukuliwa hatua kali kisheria kwani kufanya hayo yote ni kutaka kuimarisha ulinzi na usalama kwa wanamorogoro pamoja na mali zao  hivyo wanatakiwa kutambua siku ya kupiga ni moja baada ya hapo wataendelea na utaratibu wao wa awali uchaguzi utakapokwisha

 

 

Akizungumzia suala la upigaji kura Dkt. Rutengwe  amewahakikishia wanamorogoro kutakuwa na ulinzi na usalama wa kutosha katika maeneo yote hivyo wananchi waondoe hofu kwa kujitokeza kwa wingi katika kupiga kura kama walivyojiandikisha ili kufanya idadi ya watu 1,259,893 waliojiandikisha kupata haki yao ya kimsingi na kuufanya Mkoa huo kuwa mfano wa kuigwa bila kuhofia lolote

Alipotakiwa kuongelea kuhusiana na maandalizi ya uchaguzi Mkuu Dkt. Rutengwe amesema katika kuchagua nafasi ya Urais, Ubunge na Udiwani maandalizi yamekamilika kilichobaki ni uhakiki wa mwisho ambao unaendelea kufanyika pia mafunzo kwa makarani waongozaji wapiga kura , wasimamizi na wasimamizi wasidizi wa vituo katika ngazi ya kata mafunzo yamekwisha tolewa kwao kwa majimbo yote 11 ndani ya Mkoa

Aidha Mkuu wa Mkoa huyo amesema kwa upande wa vifaa vya uchaguzi amesema Morogoro ina vituo vya upigaji kura 3,957 hivyo vifaa kama masanduku ya kura, karatasi za kupigia kura, mihuri na vibweta , wino maalum usiofutika na vinginevyo tayari vimekwisha wasili na kusambazwa katika vituo husika

Aidha Dkt.Rutenge amesisiza atasimamia Sheria na Taratibu kutoka kwa Mh Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuwaasa wanamorogoro waliojiandikisha kupiga kura kuwa wastaarabu wanapomaliza kupiga kura warudi majumbani kwao kusubiria matokeo hakuna haja ya kuendelea kukaa eneo la upigaji kura kwani wanotakiwa kuwapo katika vituo hivyo ni wale wanaofahamika kisheria ili kuondokana na ghasia zisizo za lazima

“kwa maana hiyo walewote  wakao kiuka maagizo na taratibu hizo watashughulikiwa kwa mujibu wa sharia bila kujali vyama vyao au nafasi aliyonayo”amesema Dkt Rutengwe

Akimalizia Mkutano huo Mkuu wa Mkoa Morogoro aliwaomba waandishi wa habari kote nchini kusaidia kuhamasisha wananchi kwenda kupiga kura siku ya jumapili na kuwakumbusha kutekeleza maagizo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kurudi nyumbani baada ya kupiga kura ili uchaguzi huo upite kwa usalama

Aidha Dkt. Rutengwe amesema waandishi wa habari ni kioo cha jamii hivyo kutumia kalamu zao kuandika habari za ukweli na zisizo na upendeleo kuonesha kuwa ni mabalozi wazuri kila wanapopita kwa kufanya habari wanazozitoa si chanzo cha vurugu nchini bali ziwe chachu ya mshikamano na kuufanya uchaguzi huu kuwa wa Amani na,huru na utulivu .

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner