MKUU WA WILAYA MOROGORO KUJITAMBULISHA CHUO KIKUU CHA SOKOINE CHA KILIMO (SUA)

 
  
   

MKUU WA WILAYA MOROGORO KUJITAMBULISHA CHUO KIKUU CHA SOKOINE CHA KILIMO (SUA)

Na:HALIMA KATALA

Mkuu  mpya   wa  Wilaya   ya  Morogoro    Mh. Muhingo Rweyemamu  ametembelea Chuo  Kikuu  cha Sokoine cha Kilimo SUA ili kujitambulisha rasmi na kupata uzoefu  pamoja  kujifunza mambo mbalimbali kuhusu chuo.

Bofya kichwa cha habari kwa habari zaidi.......

Aidha Rweyemamu ameongeza kuwa kwa kuwa SUA   kinajishughulisha na maswala ya kufundisha  kilimo na sayansi zake ameahidi kutumia ziara hiyo ya mafunzo kwa  ajili ya  kuja  kuwakwamua wakulima pamoja na wafugaji.

Kwa  upande wake Makamu wa Mkuu wa Chuo Prof. Gerald Monela   ametoa shukrani zake  za dhati kwa niaba ya Chuo, kwa ujio wa Mkuu huyo  wa Wilaya na kusema kuwa ni   faraja kwa chuo  kukichagua kuwa Tasisi ya kwanza kuitembelea .

Aidha Prof, Monela  amezitaja changamoto zinazoikabili Taasisi hii kuwa ni pamoja na uvamizi wa  maeneo ya chuo kwa wananchi wanaoyazunguka maeneo hayo kwa kujenga nyumba, kulima mashamba na wengine kuyageuza kuwa maeneo ya kuchimbia mchanga.

Prof. Monela ameyataja maeneo yenye migogoro mikubwa na wananchi kuwa ni pamoja na eneo lililoko Lukobe ambapo amesema kuwa tayari kesi iko mahakamani  kuhusu swala la mgogoro ya ardhi ya Chuo na wananchi wa lukobe  na pia malalamiko haya walishayafikisha kwa mkuu wa wilaya aliyepita Bw, Saidi Amanzi.

Akizungumzia malalamiko hayo ya chuo mkuu huyo wa wilaya ameahidi kuyashughulikia matatizo yote yanayoikumba Taasisi hii na amesema kinachotakiwa ni ushirikiano mkubwa baina ya Chuo na  ofisi yake ili kufanikisha suala zima la kumaliza migogoro ya ardhi inayoendelea baina ya Chuo na wananchi wa Lukobe.

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner