HALI YA USAFI SOKO KUU LA MKOA MOROGORO NI YA KURIDHISHA

      

HALI YA USAFI SOKO KUU LA MKOA MOROGORO INAKURIDHISHA

Na: AYOUB  MWIGUNE

Hali ya usafi ndani ya soko kuu la mkoa wa Morogoro imekuwa ni ya kuridhisha kutokana na jitihada mbalimbali zilizofanywa na viongozi pamoja na wafanyabiashara waliopo ndani ya soko hilo kusafisha mitaro iliyokuwa imeziba.

 

 Bofya hapa kwa Habari zaidi.......

Akizungumza na SUAMEDIA kuhusiana na usafi huo Bwana Rashidi Chande  ambaye ni katibu mkuu wa soko hilo amesema suala la usafi limekuwa ni la kuridhisha kutokana  na jinsi walivyoweza kuweka taratibu za kufanya usafi ndani ya soko ambapo kila mfanyabiashara anatakiwa kuchangia kiasi cha shilingi hamsini ili kukiwezesha kikundi kazi kuweza kufanya kazi za kuzoa takataka kwa ufanisi.

 

Ameendelea kusema kuwa usafi kwao imekuwa kauli mbiu ambayo kila mfanyabiashara lazima aifuate na kwamba kwa sasa wamekuwa wakishirikiana na manispaa ya Morogoro ili kuhakikisha soko linakuwa safi wakati wote.

 

Kuhusiana na namna gani wanajikinga na kipindupindu bw. Chande amesema kwa sasa wanahakikisha kila mfanyabiashara anaweka mazingira ya eneo lake katika hali ya usafi pamoja na kudhibiti watu kujisaidia pembezoni mwa soko ambapo pia amewaomba wateja wanaofika katika soko hilo kuzingatia usafi kwa kutupa taka katika mapipa ya uchafu. 

 

Aidha bwana chande amesema changamoto kubwa wanayokutana nayo kuhusiana na usafi ni kwa wafanya biashara wengi kutochangia gharama ya usafi ambayo ni shilingi hamsini kwa siku kwa kila mfanyabiashara ili kuweza kuwalipa kikundi cha usafi ndani ya soko hali inayowalazimu viongozi kutoa fedha zao za mfukoni.

 

Naye bwana Sulemani Nesto ambaye ni mfanyabiashara ndani ya soko hilo amewataka wafanyabiashara wenzake ambao hawataki kuchangia gharama za usafi kuacha tabia hiyo na kudumisha ushirikiano ili kuleta maendeleo ya soko hilo.

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner