WANAWAKE WASHAURIWA KUFUGA SAMAKI KUODOKANA NA UMASKINI

   

Na: FARIDA MKONGWE

Wakulima na wafugaji wameshauriwa kujihusisha na shughuli za ufugaji wa samaki kwa kuwa ufugaji huo una faida kubwa na unaweza kuwa ni chanzo cha kuondokana na umaskini.

 

Bofya hapa kwa Habari zaidi........

 

Ushauri huo umetolewa na mfugaji wa samaki ambaye ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) katika fani ya Uzalishaji wa Viumbehai katika maji  bi. Asteria Mboya wakati akizungumza na SUAMEDIA kuhusu faida mbalimbali anazozipata kutokana na ufugaji wa samaki.

 

“Mimi nawashauri wafugaji wenzangu na hasa wanawake wajitume kwa hali na mali kufuga samaki, binafsi ufugaji huu umenisaidia sana kuendesha maisha yangu nimeepukana na maisha tegemezi na pia ufugaji wa samaki umeniwezesha kukutana na watu mbalimbali katika sekta ya kilimo na kubalishana nao mawazo ya namna ya kuendesha kwa faida mradi huu wa ufugaji samaki”, alisema bi. Asteria.

 

Katika hatua nyingine mfugaji huyo wa samaki amewataka wafugaji wanzake  kuwa wavumilivu katika hatua za awali za ufugaji na kutokata tamaa pindi wanapokutana na changamoto mbalimbali na kwamba cha msingi ni kufuata na kuzingatia maelekezo ya wataalamu ili waweze kufanikiwa na kupata faida.

 

 

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner