ZIARA YA KUANGALIA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI MBALIMBALI SUA

Na: Fransis Mwakatenya

Menejimenti ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, SUA ikiongozwa na Makamu wa Mkuu wa Chuo,Prof. Raphael Chibunda mnamo 31 Octoba 2018 imefanya ziara ya kuangalia utekelezaji wa shughuli mbalimbali ikiwemo miradi na ukaguzi wa mipaka ya Chuo katika maeneo yanayovamiwa na wananchi hususani Lugala, Lukobe na Lukobe Juu.

IMG 20181101 WA0007Msafara wa menejimenti ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA ukiwasili katika moja ya eneo kwa kufanya ukaguzi

Aidha ziara hiyo imefikia miradi mbalimbali iliopo chuoni kwa lengo la kuangalia uboreshaji pamoja na ukarabati unaoendelea katika Hostel ya Unit One unaofanywa na TBA, Gowdown la kuhifadhi mizigo na kiwanda kinachotengeneza thamani Vuyusile Min.

IMG 20181101 WA0013Makamu wa Mkuu wa Chuo  SUA Prof. Raphael Chibunda akiwa pamoja na viongozi wa Chuo SUA,  wakijadili jambo mara baada ya kufika katika moja la eneo walilotembelea

Vilevile timu hiyo ilkagua kisima cha maji kinachochimbwa kwa ajili ya kuhudumia wanafunzi na wakazi wa Kampasi ya Solomoni Mahlangu.

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner