JAMII YAASWA KUTUMIA BAMBOO KUONDOKANA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA

Na.Halima KatalaMbozi


Wananchi wametakiwa kuelewa kwa usahihi kuhusu matumizi ya mmea aina ya Bamboo (Mwanzi) katika utengenezaji wa samani ili kuondokana na uharibifu wa Mazingira kwani ni mmea wenye matumizi mengi kuliko mmea wowote duniani. 

Hayo yameelezwa na Mhadhiri msaidizi kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo (SUA) Bw. Paul Lyimo wakati akifanya mahojiano kupitia kipindi cha Mchakamchaka   kinachorushwa na SUAFM.

Picha na mtandao

Bw. Lyimo amesema Chuo cha Sokoine cha Kilimo kimekuwa kikifanya utafiti wa mmea huo na kuona ni namna gani unaweza kumsaidia mkulima na mwananchi katika uzalishaji wa Malighafi mbalimbali hasa Samani.

Pia Bw. Lyimo amewashauri wakulima kujikita katika kilimo cha Bamboo kwani kiutaalamu kuna Bamboo ambazo zina wigo mpana wa ukuaji mfano aina ya Savrugarisi kwani inaweza kukua sehemu yoyote nchini Tanzania japo ukuaji wake unatofautiana, pia haichukui muda mrefu hadi kuvunwa tofauti na miti mingine ambayo inasumika katika matumizi ya utengenezaji wa Samani.

Picha na mtandao

Aidha Lyimo amesema katika nchi ambazo zimeendelea kama China watu wake wanatumia mmea wa Bamboo katika utengenezaji wa karatasi nan chi ya Ghana ambao wanatumia mmea huo katika kutengenezea Baiskeli hivyo ni vyema jamii sasa ikatambua umuhimu wa zao hilo.

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner