WAKAZI WA MANISPAA YA MOROGORO KUPATA FURSA YA MATIBABU TOKA MAREKANI

      

Na: IRIMINA MATERU

Shirika la Marekani linalojihusisha na huduma ya kutoa madawa kwa kukishirikiana na Kanisa la Kiimani lililopo Kola B mkoani Morogoro limewashukuru madaktari wa  Hospital ya Mkoa wa Morogoro kwa ushirikiano kwa kutoa huduma ya kiafya mkoani Morogoro .

 

Bofya hapa kwa Habari zaidi.......

Akizungumza na SUAMEDIA Mchungaji wa kanisa hilo Jerry Wyatt amesema kuwa lengo la kutoa huduma hiyo ni kusikiliza matatizo ya kimwili, kuwasaidia na kuwapatia tiba wagonjwa  ili waweze kuondokana na magonjwa yanayowakabili.

 “Watu wengi wana matatizo wanasumbuliwa na macho, BP, uzito, ulaji hauzingatiwi, kuna matatizo ya magoti, kuna matatizo mbalimbali na tangu tumeanzisha huduma hii wengi wameitika kwenye miwani kwa hiyo inavyoonekana wengi wanasumbuliwa na macho lakini wanashindwa pesa za kwenda kupima na kupata miwani hivyo hapa huduma  ni bure na nashukuru pia watu wamejitokeza” Alieleza mchungaji Jerry

Aidha Mchungaji huyo amewataka wananchi kuzingatia ulaji wa vyakula na kujitahidi kunywa maji mengi kwani itawasaidia kujihepusha kunywa vinywaji vyenye sukari mara kwa mara  kwa kufanya hivyo itawasaidia kukwepa matatizo kwa upande wa afya.

Kwa upande wake Mtalaam wa macho na miwani Bwana Leonard Machange amesema mwitikio wa watu katika huduma hiyo ni mkubwa hasa kwa wagonjwa wa macho hivyo amewashauri watanzania wote kupenda kujitokeza mara kwa mara katika Vituo vya Afya na upimaji afya zao ili kuweza kukabiliana na magonjwa mbalimbali.

Hata hivyo jamii imepokea vyema huduma hiyo na kulishukuru Shirika hilo kwa matibabu wanayoyapata na kusema kuwa wanafurahi kwani shirika hilo limewapunguzia  gharama ya kwenda Hospitali  hali ambayo inayowakwamisha walio wengi na kushindwa kupata matibabu wanayostahili.

SUAMEDIA-BANNER

suamedia banner